Home news BAADA YA KUONA SIMBA WAMELETA KOCHA WA ‘SOKA BIRIANI’..NABI AKUNA KICHWA..KISHA AFUNGUKA...

BAADA YA KUONA SIMBA WAMELETA KOCHA WA ‘SOKA BIRIANI’..NABI AKUNA KICHWA..KISHA AFUNGUKA HAYA…


KOCHA wa Yanga, Nasrredine Mohamed Nabi, amefunguka kuwa anahitaji timu yake iwe na uwezo mkubwa zaidi wa kumiliki mpira na kuwa na rekodi ya kupiga pasi nyingi kwenye kila mechi.

Nabi alisema soka la kisasa limebadilika sana kwa sababu timu yenye uwezo wa kumiliki mpira muda mrefu na kupiga pasi nyingi ndiyo huwa na nafasi ya kushinda mchezo kwa sababu wachezaji wanaongeza kujiamini.

Akizungumza hivi karibuni, Nabi alisema timu yake imekuwa na uwiano mzuri kwenye kupiga pasi na kumiliki mpira, ila bado kuna kitu kidogo hakijakaa sawa na anakifanyia kazi baada ya muda mfupi timu hiyo itakuwa tishio zaidi kwenye pasi.

“Nahitaji timu yangu na wachezaji wawe na uwezo wa kumiliki mpira zaidi ya sasa. Ubora wa kupiga pasi uwe juu zaidi na tuwe kati ya timu ambazo zina idadi kubwa ya pasi.

“Timu inayofanya hivyo hujiweka kwenye mazingira mazuri ya kushinda mchezo. Kadiri unavyokaa na mpira muda mrefu timu inaongeza kujiamini na kumchanganya mpinzani, hicho ndiyo tunahitaji,” alisema Nabi.

Kwa miaka ya hivi karibuni soka la pasi nyingi limekuwa likichezwa zaidi na Simba SC ambapo walifikia hatua ya kulipachika jina la utani la Soka Biriani.

Hata hivyo, katika kuendeleza soka hilo,Simba SC imejinasibu kuwa kocha wao Mpya Mhispania Pablo Franco ni muumini wa soka hilo, haswa ukizingatia taifa alilotoka la Hispania kuwa ni watu wanaolimudu soka la pasi nyingi.

SOMA NA HII  YANGA YAPIGWA FAINI YA MILIONI 3 NA BODI YA LIGI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here