Home news FT: TANZANIA 0-3 DR CONGO…A-Z JINSI STARS ‘WALIVYONYANYASWA’ UWANJANI..MATUMAINI BADO…

FT: TANZANIA 0-3 DR CONGO…A-Z JINSI STARS ‘WALIVYONYANYASWA’ UWANJANI..MATUMAINI BADO…


TIMU ya Taifa ‘Taifa Stars’ imeshindwa kutamba kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya kufungwa mabao 3-0, dhidi ya DR Congo katika mchezo wa kufuzu kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.

Mabao ya Gael Kakuta dakika ya sita, Nathan Fasika dakika ya 66, pamoja na la Ben Malango yametosha kuizamisha Stars iliyokuwa ikihitaji ushindi kwenye mchezo wa leo ili kujiweka katika nafasi nzuri.

Kipindi cha pili Kim Poulsen alifanya mabadiliko kwa kumtoa Novatus Dismas na nafasi yake kuchukuliwa na Mzamiru Yassin ili Kuongezea nguvu kwenye safu ya kiungo.

Mabadiliko hayo yalileta uimara kwenye safu ya kiungo tofauti na ilivyokuwa katika kipindi cha kwanza ambacho tulizidiwa kwenye eneo hilo.

Kwa upande wa DR Congo waliwatoa Dieumerci Mbokani na Akolo Ababa huku nafasi zao zikichukuliwa na Rebano Neeskens pamoja na Edo Kayembe.

Dakika ya 59, Poulsen aliwatoa Kibu Denis na Kennedy Juma huku nafasi zao zikichukuliwa na John Bocco na Erasto Nyoni ili kuongeza ufanisi kwenye kwenye safu ya ulinzi na ushambuliaji.

Huku DR Congo ikimtoa mfungaji wa bao la kwanza Gael Kakuta ambapo nafasi yake ilichukuliwa na Yannick Bolasie anayechezea klabu ya Çaykur Rizespor ya nchini Uturuki.

Mabadiliko hayo yalileta tija kwa wageni kwani dakika ya 66, Congo ilipata bao la pili baada ya mlinzi Nathan Fasika anayechezea klabu ya Cape Town City FC ya Afrika Kusini kuunganisha mpira safi uliopigwa na Arthur Masuaku.

Stars iliendelea kufanya mabadiliko kwa kuwatoa Feisal Salum, Shomari Kapombe huku nafasi zao zikichukuliwa na Kibwana Shomari na Reliant Lusajo.

Mnamo dakika ya 75, John Bocco angeipatia bao Stars baada ya kupiga kichwa safi kilichookolewa na golikipa Kiassumbua Joel.

Dakika ya 85, Congo ilipata bao la tatu kupitia kwa Ben Malango anayechezea klabu ya Sharjah ya uarabuni na kuwafanya Stars kuwa na mlima wa kupanda kwenye harakati za kufuzu Kombe la Dunia Mwakani.

Baada ya mchezo huu Stars itashuka Uwanjani Novemba 14, kuhitimisha mchezo wa mwisho nchini Antananarivo dhidi ya Madagascar.

SOMA NA HII  LILE DILI LA STRAIKA MCAMEROON KUTUA SIMBA 'UPDATE' HII HAPA....MBRAZILI ALETA KOCHA MSAIDIZI MPYA..

Matokeo haya yanaifanya Stars kusalia na pointi saba ikiwa nafasi ya pili huku DR Congo ikipaa kileleni mwa msimamo wa kundi ‘J’ kwa kufikisha alama nane baada ya timu zote kucheza michezo mitano.