Home news IMEFICHUKA…KOCHA ATAJA SABABU ZA KAKOLANYA KUENDELEA KUSUGUA BENCHI SIMBA ..

IMEFICHUKA…KOCHA ATAJA SABABU ZA KAKOLANYA KUENDELEA KUSUGUA BENCHI SIMBA ..


MILTON Nienov aliyekuwa kocha wa makipa ndani ya Simba ameweka wazi kuwa sababu kubwa iliyomfanya kipa namba mbili wa timu hiyo, Beno Kakolanya kushindwa kupata nafasi kikosi cha kwanza ndani ya Simba ni ugumu wa nafasi hiyo katika kufanya mabadiliko.

Raia huyo wa Brazil amebainisha kuwa kuna sehemu ambazo ni jambo rahisi kufanya mabadiliko ila eneo la kipa huwa linakuwa gumu kutokana na kumlinda yule anayeanza.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Nienov alisema kuwa katika kazi ya kuwapa nafasi makipa ni lazima kuzingatia utimamu wa mwili pamoja na utendaji wake kwenye kazi ambayo huwa anaifanya.

“Kuna makipa wazuri Simba ikiwa ni pamoja na Kakolanya, Kisubi (Jeremiah) lakini namba moja amekuwa akitumika mara kwa mara Manula huku Kakolanya akikaa benchi, na sababu ni ugumu wa nafasi katika kufanya kazi.

“Ukiwa mwalimu kuna yule kipa namba moja na kuna chaguo la mwalimu na mara nyingi namba moja huwa anapenya kikosi cha kwanza jumla,” alisema Mbrazili huyo aliyechimbishwa ndani ya Simba Oktoba 26, kwa kile kilichoelezwa ni makubaliano ya pande zote mbili.

Wakati anasepa aliacha Simba ikiwa imecheza mechi tano, Manula amecheza tano huku Kakolanya akiwa hajacheza hata moja.

SOMA NA HII  MORRISON AWAPA AKILI YANGA