Home news IMEFICHUKAA..HII NI ZAIDI YA KUFURU…SIMBA KUMLIPA ZAIDI YA BILIONI 1 KOCHA MPYA..MLOLONGO...

IMEFICHUKAA..HII NI ZAIDI YA KUFURU…SIMBA KUMLIPA ZAIDI YA BILIONI 1 KOCHA MPYA..MLOLONGO UKO HIVI..


WAKATI Kocha Mkuu mpya wa Simba, Pablo Franco, akitarajiwa kutua nchini leo kabla ya kutambulishwa kesho na kuanza kazi mara moja, ataigharimu timu hiyo Sh. milioni 768 kama mshahara wake tu, kwa kipindi cha mkataba wa miaka miwili atakaosaini, imefahamika.

Franco ambaye ni mzaliwa wa jijini Madrid, Hispania, mbali na mshahara huo pia atavuta jumla ya Sh. milioni 138 kwa mwaka kama bonasi endapo atatimiza malengo yake aliyowekewa na waajiri wake hao.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani , Franco atakuwa akilipwa Dola za Marekani 14,000 kwa mwezi sawa na Sh. milioni 32 za Tanzania huku pia akigharamiwa tiketi ya ndege ya kurejea kwao na kurudi nchini.

“Bonasi atakazopata ni Sh. milioni 23 endapo atatwaa ubingwa wa Ligi Kuu, na kiasi kama hicho endapo ataiwezesha timu kufika robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, lakini atalipwa Sh. milioni 46 akituwezesha kufika nusu fainali ya michuano hiyo na tukifika fainali atalipwa pia bonasi ya Sh. milioni 46,” kilieleza.

Franco mwenye umri wa miaka 41, ana leseni ya UEFA-Pro na anatua Simba akitokea Al-Qadsia ya Kuwait, lakini amewahi kuwa kocha msaidizi wa Real Madrid mwaka 2018 pia akiifundisha Getafe ya Ligi Kuu Hispania mwaka 2015.

“Miaka saba iliyopita, nilipata ushindi wangu wa kwanza kama kocha mkuu katika Uwanja wa Alfredo Di Stefano, kwa kuifunga Real Madrid Castilla ikinolewa na #Zidane [Zinedine]. Kumbukumbu nzuri,” Franco ameandika katika mtandao wake wa twitter akiambatanisha picha wakiwa na Zinedine Zidane.  

SOMA NA HII  WORLD CUP: ALIYESHANGILIA KAMA RONALDO MBELE YAKE AFUNGUKA SABABU YA KUFANYA HIVYO..