Home news KISA HUKUMU YA MORRISON…MWAKALEBELA AIBUKA NA JIPYA YANGA…AWATAKA MASHABIKI WASAHAU….

KISA HUKUMU YA MORRISON…MWAKALEBELA AIBUKA NA JIPYA YANGA…AWATAKA MASHABIKI WASAHAU….


Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Young Africsns Fredrick Mwakalebela amesema klabu hiyo imetii agizo la kumlipa Kiungo Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Bernard Morrison, lililotolewa na Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo ‘CAS’.

Young Africans iliamrishwa kumlipa Morrison fidia ya Swis 5,000 ambazo ni sawa na Shilingi Milioni 12,396,787, baada ya kushindwa kesi iliyokua ikiendeshwa kwenye Mahakama hiyo.

Hati ya hukumu iliyokuwa na kurasa 29 imeeleza kuwa ushahidi uliotolewa na Young Africans juu ya mkataba mpya uliotolewa na klabu hiyo, ulikuwa na makosa mengi na kushindwa kuwa na ushahidi wa kutosha kama ulisainiwa na Morrison.

Mwakalebela amesema kuwa, katika hukumu kuna maamuzi mawili kushinda na kushindwa, hivyo Wanayanga wasahau hayo na badala yake kurejesha nguvu katika Ligi Kuu Bara.

“Wao (Simba) wametushinda CAS, basi na sisi Yanga tunatakiwa kuwashinda uwanjani kwa matokeo mazuri tutakapokutana nao Desemba 11, mwaka huu katika mchezo wa ligi.”

“Tulikuwa tuna matarajio makubwa ya kushinda kesi hii CAS, hiyo ndiyo sababu ya kutumia gharama kubwa ya kukata rufaa CAS baada ya maamuzi ya utata TFF.”

“Hivyo Wanayanga tunatakiwa kuungana kwa pamoja katika kuisapoti timu yetu katika michezo ya ligi na kikubwa kuchukua ubingwa huo katika msimu huu na Kombe la FA,” amesema Mwakalebela.

SOMA NA HII  KISA KUFUZU KOMBE LA DUNIA ...TIMU ZA TAIFA ZAJAZWA MABILIONI YA PESA...WAZIRI MKUU AFUNGUKA A-Z...