Home news KUELEKEA MECHI DHIDI YA MBEYA KWANZA…MASTAA YANGA WALA KIAPO…MAYELE ASHINDWA KUJIZUIA…

KUELEKEA MECHI DHIDI YA MBEYA KWANZA…MASTAA YANGA WALA KIAPO…MAYELE ASHINDWA KUJIZUIA…

 


MASTAA wa Yanga ni kama wamekula kiapo kuhakikisha wanaibuka na ushindi dhidi ya Mbeya Kwanza leo Jumanne kutokana na kuweka wazi kuwa wanahitaji pointi tatu muhimu dhidi ya wapinzani wao kutoka Mbeya.

Yanga juzi Jumapili iliwasili tayari mkoani Mbeya kwaajili ya maandalizi ya mchezo huo unaotarajiwa kufanyika kesho katika Uwanja wa Sokoine jijini humo ambapo Mbeya Kwanza watakuwa wenyeji wa Yanga.

Kuelekea katika mchezo huo klabu ya Yanga ndiyo vinara wa ligi wakiwa wamejikusanyia jumla ya alama 16 mara baada ya kuibuka na ushindi katika michezo 5, huku mmoja wakitoka sare dhidi ya Namungo kwa bao 1-1.

Kiungo wa timu hiyo Feisal Salum alisema kuwa malengo yao wakiwa kama wachezaji ni kuhakikisha wanaibuka na ushindi mara baada ya kupata sare katika mchezo uliopita.

“Mchezo uliopita tulipata sare dhidi ya Namungo,tunashukuru ambacho tulikipata lakini kuelekea katika mchezo dhidi ya Mbeya Kwanza hakuna ambacho tunahitaji zaidi ya ushindi, tunafahamu tunakutana na timu ngumu lakini tutapambana kwa ajili ya ushindi.

Naye mshambuliaji Fiston Mayele kuelekea katika mchezo huo alisema kuwa :“Unajua kila ambaye tunacheza naye anatamani kuona anatafunga Yanga, sisi hatupo tayari kwa hilo na ndiyo maana tunatakiwa kuuona kila mchezo ambao upo mbele yetu kuwa ni fainali kwetu naamini kupitia hilo tutapata matokeo mazuri ambayo ni ushindi,”alisema mshambuliaji huyo.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA AZAM...NABI KAAMUA KULA SAHANI MOJA NA BANGALA...MOLOKO APEWA MBINU MBADALA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here