Home news MANARA:..KUNA ZAMBI INATENGEZWA KUHUSU MWAMNYETO…HATUWEZI KUISHI KWA KUKARIRI…

MANARA:..KUNA ZAMBI INATENGEZWA KUHUSU MWAMNYETO…HATUWEZI KUISHI KWA KUKARIRI…


MSEMAJI wa klabu ya Yanga, Haji Manara amemsifu kocha wa timu hiyo, Nassredine Nabi kwa namna ambavyo timu hiyo inavyocheza soka lake la pasi nyingi.

Yanga katika mchezo wao uliopita dhidi ya Azam walipiga pasi 23 kuanzia kwa kipa mpaka wachezaji wa mbele na Jesus Moloko aliweka wavuni bao la pili.

Manara amesema mpaka sasa katika timu yao wachezaji wao wote wanapiga pasi na hilo lilianza kujitokeza katika mchezo wao dhidi ya KMC.

“Tumepata ushindi wa mechi tano na haikuwa rahisi ilikuwa ni ushindi wa jasho na damu. Sisi sio tunapiga pasi tu kama wengine wanaopiga pasi wakiwa eneo lao, sisi tunapiga pasi na kwenda mbele.

“Kuna watu wanasema hata mwaka jana tuliongoza ligi baadae tukaachia, hatuwezi kuishi kwa kukariri kama mnakariri mbona hamkariri kuwa Yanga ni bingwa mara 27 karirini na hilo.

”Kuna dhambi naona inaanza kutengenezwa, wanaongelewa Aucho, Feisal na Bangala lakini husikii wakiongelewa Dickson Job wala Mwamnyeto ambao wamecheza dakika zaidi ya 400 na hawajaruhusu goli. Kwangu mimi Mwamnyeto sio mlinzi ni Holding Defender. Sisi tuna Timu, yule Diara ana side mirror, yaan anaona mbele kabla hata ya kupokea mpira.

SOMA NA HII  MASTAA AZAM FC WAFUNGUKA ISHU YA KUTAKIWA YANGA SC...MMOJA ACHOMOA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here