Home news MUKOKO..NTIBAZONKIZA KIKAANGONI YANGA…NABI AKABIDHIWA RUNGU LA MAAMUZI..INJINIA HERSI AWAKATA KIAINA…

MUKOKO..NTIBAZONKIZA KIKAANGONI YANGA…NABI AKABIDHIWA RUNGU LA MAAMUZI..INJINIA HERSI AWAKATA KIAINA…


KIKOSI cha Yanga kinaendelea kujifua kujiandaa na mechi zao zijazo za Ligi Kuu Bara, huku kocha wao, Nasreddine Nabi akikomaa nao gym kabla ya kurejea kuwapigisha tizi la uwanjani, lakini kuna mastaa wasiopungua sita wapo kwenye vita nzito kabla ya dirisha dogo halijafunguliwa.

Ipo hivi. Ubora wa kikosi cha Yanga unawaweka kikaangoni mastaa hao sita kabla ya dirisha dogo la usajili halijafunguliwa mwezi ujao na kufungwa Januari mwakani.

Wachezaji hao sita wameonekana kushindwa kulishawishi benchi la ufundi la Yanga kuwapa nafasi ya kucheza katika mechi sita zilizopita za Ligi Kuu na hivyo wana michezo sita mbele ya kujitetea kabla ya dirisha dogo vinginevyo wanaweza kufunguliwa milango.

Mechi hizo sita ni dhidi ya Namungo FC, Mbeya Kwanza, Simba, Tanzania Prisons, Biashara United na Dodoma Jiji FC.

Licha ya Kamati ya Usajili ya Yanga kudai ni mapema kuzungumzia suala la usajili kwa sasa, ni wazi kwamba wachezaji hao sita wanapaswa kujituma vilivyo ili waanze kupewa muda wa kucheza vinginevyo watajikuta katika wakati mgumu.

“Ni mapema sana saizi kuzungumzia usajili kwa sababu timu inashinda na ubora wa wachezaji unaonekana, kuhusu kusajili au kutokusajili inategemeana na uhitaji wa kocha,” alisema Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Injinia Hersi Said.

Mabeki wawili wa kushoto, Adeyum Saleh na Yassin Mustafa ndio walio katika presha kubwa zaidi kutokana na ushindani wa namba walionao kutoka kwa wachezaji wengine wawili wanaotumiwa katika nafasi hiyo.

Kocha Nabi amekuwa akimtumia zaidi kiraka Kibwana Shomary kucheza upande huo huku kwa sasa chaguo la pili akionekana ni David Bryson ambaye awali hakuonekana uwanjani kutokana na majeraha.

Uwepo wa wachezaji wanne wanaocheza katika nafasi moja unatengeneza mazingira magumu kwa mmoja wapo kati ya Yassin na Adeyum kubakia Yanga kwa muda mrefu na huenda mmojawapo au wote wakapunguzwa au kutolewa kwa mkopo kupisha usajili wa wachezaji wa nafasi nyingine.

Upande wa beki wa kulia, Paul Godfrey ‘Boxer’ pia anatakiwa kufanya kazi ya ziada kuishawishi Yanga ibaki naye kwani anaonekana kushindwa kuhimili ushindani wa Shaban Djuma na Kibwana Shomari.

SOMA NA HII  JEMBE LA KAZI YANGA LAANZA MATIZI, MANULA ANAJUA SHUGHULI YAKE

Wengine walio katika preha kubwa kwa sasa na hapana shaka wanalazimika kupambana vilivyo ili kulikwepa panga ni winga Deus Kaseke, kiungo Saido Ntibazonkiza na mshambuliaji Ditram Nchimbi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here