Home Burudani TWAHA KIDUKU ‘AMKIMBIA’ MWAKINYO…DULLA MBABE NDIO BASI TENA…

TWAHA KIDUKU ‘AMKIMBIA’ MWAKINYO…DULLA MBABE NDIO BASI TENA…

 


NI kama bondia Twaha ‘Kiduku’ Kassim amemkimbia Hassan Mwakinyo baada ya mtandao wa ngumi za kulipwa wa dunia (Boxrec) kutoa viwango vipya vya ubora wa mabondia nchini.

Katika viwango hivyo vya mabondia wa kila uzani (pound for pound), Kiduku ameporomoka kutoka nafasi ya tano hadi ya nane.

Mwakinyo ameendelea kung’ang’ania nafasi ya kwanza kwenye uzani wake wa super welter na nafasi hiyo kwenye pound for pound ya Tanzania.

Kiduku bondia namba moja kwenye uzani super middle aliyewahi kutamani kuzichapa na Mwakinyo ameporomoka kwa nafasi tatu zaidi, akiwa na muendelezo wa kuporomoka tangu mwaka jana.

Bondia huyo mwaka jana mwanzoni alitajwa na Boxrec kuwa namba mbili nyuma ya Mwakinyo kabla ya kuporomoka hadi nafasi ya tatu, kisha ya tano na sasa ni wa nane akiwa na pointi 1.561 na nyota mbili, akizidiwa kwa pointi 20 na Mwakinyo mwenye pointi 22.21 na nyota nne.

Ibrahim Class bondia namba moja kwenye uzani wa super feather amekamata nafasi ya pili kwenye pound for pound akiwa na pointi 6.972 na nyota tatu huku Fadhili Majiha bondia namba moja kwenye uzani wa bantam mwenye pointi 2.781 akihitimisha tatu bora.

Wengine walioingia 10 bora ni Salim ‘Mtango’ Jengo, Tony Rashid, Innocent Evarist, Hamisi Maya, Kiduku, Loren Japhet na Mukhsin Swalehe ‘Mastik the Don’.

Mastaa wengine waliotajwa kwenye viwango hivyo na nafasi walizokamata kwenye mabano ni Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ (18), Nasibu Ramadhani (14), Francis Miyeyusho (17), Cosmas Cheka (17) Allan Kamote (24), Suleiman Kidunda (35), Mfaume Mfaume (40), Said Mbelwa (80), Kanda Kabongo (99), Japhet Kaseba (111), Awadh Tamim (163) na bondia anayekamata mkia nchini ni Abubakar Temihanga (534).

SOMA NA HII  ISHU YA MWAKINYO KUPIGWA JANA...MJADALA WA KUUZA MECHI WAIBUKA...MASHABIKI UINGEREZA WAMTOLEA 'POVU'...