Home news BAADA YA DABI KUISHA…KOCHA YANGA ASHINDWA KUJIZUIA KWA MANULA..ADAI NI MAMBO YA...

BAADA YA DABI KUISHA…KOCHA YANGA ASHINDWA KUJIZUIA KWA MANULA..ADAI NI MAMBO YA MPIRA..

 


NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa mikono ya kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula iliwazuia kupata ushindi kwenye mchezo wao wa ligi.

Juzi, Uwanja wa Mkapa, Yanga ilikuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya Simba lakini ubao wa ulisoma Simba 0-0 Yanga na kufanya timu hizo kugawana pointi mojamoja.

Nabi amesema kuwa isingekuwa ni Manula basi wangeifunga Simba kwenye mchezo huo kwa kuwa walitengeneza nafasi nyingi ambazo zilikuwa zinawapa uhakika wa ushindi.

“Kipa wao yule wa Simba, (Aishi Manula) amefanya kazi kubwa kwenye kuokoa mipira yetu, kwa mfano kuna mpira ulipigwa na Said Ntibanzokiza unadhani asingekuwa imara nini kingetoa zaidi ya kuwa bao?

“Itoshe kusema kwamba ni kipa mzuri na ukitegemea kwamba ni kipa ambaye anadaka kwenye timu ya taifa, (Taifa Stars). Ni mambo ya mpira huwa yanatokea lakini ninawezakusema kwamba wachezaji wangu walicheza vizuri,” alisema Nabi.

Manula anafikisha jumla ya mechi nane kukaa langoni huku akiwa ameruhusu kufungwa mechi mbili mabao mawili na kwenye mechi sita alikuwa shujaa kwa kuwa hakufungwa.

SOMA NA HII  IMEFICHUKA...KUMBE MAGOLI 17 YA MPOLE KWENYE LIGI YANA SIRI NZITO NYUMA YAKE...MIPANGO YOTE ILIKUWA HIVI...