Home news BAADA YA KUICHAKATA GEITA GOLD KIBABE..SIMBA YAITANGAZIA MAANGAMIZI KWA ANAYEFUATA…

BAADA YA KUICHAKATA GEITA GOLD KIBABE..SIMBA YAITANGAZIA MAANGAMIZI KWA ANAYEFUATA…

 


Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Simba na Geita Gold umemalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Bao la Peter Banda dakika ya tisa ya kipindi cha kwanza na la Mzamiru Yassin dakika ya 60, yametosha kuwapa pointi tatu huhu Geita wakipata bao la kufutia machozi kupitia Juma Mahadhi dakika ya 66.

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ambapo Geita iliwatoa Amos Kadikilo na Raymond Massota nafasi zao zikichukuliwa na Venancy Ludovic na Jeremiah Rubanguka.

Kwa upande wa Simba iliwatoa Ibrahim Ajibu na Larry Bwalya huku nafasi zao zikichukuliwa na Bernard Morrison na Mzamiru Yassin.

Mabadiliko hayo yalikuwa ya faida kwa Simba ambapo dakika ya 60, Mzamiru Yassin alifunga bao la pili ikiwa ni mpira wa kwanza kugusa tangu aingie.

Simba iliendelea kufanya mabadiliko wakitoka Peter Banda, John Bocco na Kibu Denis huku Meddie Kagere, Erasto Nyoni na Pascal Wawa wakichukua nafasi zao.

Geita wanapoteza mchezo wa nne msimu huu baada ya kufungwa mabao 2-0, na Namungo FC Septemba 27, wakafungwa bao 1-0, na Yanga Oktoba 2, wakapoteza bao 1-0, dhidi ya Azam FC Novemba 2, na wa leo dhidi ya Simba.

Katika michezo saba iliyocheza Simba imeshinda mitano dhidi ya Dodoma Jiji bao 1-0, Oktoba Mosi, Polisi Tanzania bao 1-0, Oktoba 27, Namungo FC bao 1-0, Novemba 3, na ushindi wa mabao 3-1, dhidi ya Ruvu Shooting Novemba 19, na wa leo dhidi ya Geita Gold.

Michezo miwili iliyobaki walilazimishwa suluhu ya 0-0 na Biashara United Septemba 28 na Coastal Union Oktoba 31.

Matokeo haya yanaifanya Simba kufikisha alama 17, pointi mbili nyuma ya vinara wa Ligi Kuu Bara Yanga yenye alama 19, kufuatia timu zote kucheza michezo saba.

Ushindi huu unaongeza hari kubwa kuelekea ‘Dabi ya Kariakoo’ itakayochezwa Disemba 11, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

SOMA NA HII  SIMBA WAPATA PIGO.... KRAMO MAMBO SIO MAMBO, DAKTARI AANIKA UKWELI WOTE