Home news BAADA YA KUONA MAMBO MAGUMU…KISUBI ASHINDWA KUJIZUIA…AOMBA KUSEPA SIMBA…

BAADA YA KUONA MAMBO MAGUMU…KISUBI ASHINDWA KUJIZUIA…AOMBA KUSEPA SIMBA…


WAKATI kipa, Aaron Kalambo akiwaomba mabosi wake wa Tanzania Prisons kuondoka kikosini kwenye dirisha hili dogo la usajili, kipa wa Simba Jeremiah Kisubi ambaye hajacheza mechi hata moja ya timu amekubali yaishe kwa kuomba kurejeshwa kwa mkopo kwa maafande hao.

Kisubi aliyekuwa chaguo la tatu nyuma ya Aishi Manula na Beno Kakolanya ndani ya Simba iliyomsajili kwa mkataba wa miaka miwili ameuandikia barua uongozi wa timu yake kuomba kumtoa kwa mkopo.

“Sina nafasi ya kucheza na natamani kuendeleza kipaji changu. Ni kweli nimefanya hivyo natarajia nitafanyiwa hivyo ili niende timu ambayo nitapata nafasi ya kucheza ili kuendeleza kipaji changu,” alisema Kisubi.

MSIKIE KALAMBO

Kalambo alijiunga na Prisons akitokea Dodoma Jiji, wakati Kisubi anarudi kwenye timu hiyo baada ya kuondoka msimu uliopita na kujiunga na Simba ambayo haijampa nafasi ya kucheza hata mechi moja.

Akizungumza hivi karibuni, Kalambo alisema ni kweli alikuwa nje ya timu lakini ni kutokana na matatizo ya kifamilia ambayo aliyaripoti kwenye timu, tofauti na inavyozungumzwa.

“Bado nipo Prisons na nimefanya mazoezi na timu Alhamisi kucheza dhidi ya Yanga, ni mipango ya mwalimu siwezi kulizungumzia hilo lakini nipo na timu baada ya kurudi baada ya kumaliza matatizo,” alisema.

Akizungumzia ishu ya kuondoka dirisha hili la usajili alikiri kuwa ni kweli endapo ombi lake litakubaliwa na uongozi baada ya kuomba kuondoka kwenda kujaribu maisha sehemu nyingine.

Alisema ana ofa nyingi kipindi hiki cha usajili na hawezi kuweka wazi ni wapi hadi mipango yake itakapokuwa sawa sambamba na ombi lake kukubaliwa.

SOMA NA HII  WAKATI YANGA WAKIZIDI 'KUSHAINI'..SHABANI DJUMA AIBUKA NA LAKE...ASISITIZA..LA SIVYO..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here