Home news KIMENUKA SIMBA….SAKHO,WAWA, KISUBI NA DUNCAN HATIMA YAO SHAKANI…MAGORI AKOLEZA MOTO..

KIMENUKA SIMBA….SAKHO,WAWA, KISUBI NA DUNCAN HATIMA YAO SHAKANI…MAGORI AKOLEZA MOTO..


HATMA ya kiungo mshambuliaji, Ousmane Sakho na beki Pascal Wawa na wenzao watatu itajulikana leo, ya kuendelea au kubakia kukipiga Msimbazi.

Wachezaji hao ndiyo wanaotajwa kuachwa katika usajili wa dirisha dogo kwa ajili ya kupata nafasi za kusajili wa kigeni.

Nyota wengine wanaotajwa kuachwa katika timu hiyo ni kiungo, Duncan Nyoni, kipa Jeremiah Kisubi, na kiungo mkabaji Abdoulswamad Kassim.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Gazeti la Championi , Kocha Mkuu wa timu hiyo, Muhispania Franco Pablo juzi Jumatatu alitarajiwa kukabidhi ripoti ya usajili.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa ripoti hiyo atakayoikabidhi ndiyo itakayoamua wachezaji wa kuachwa na kusajili ambao amewapendekeza katika dirisha dogo.

Aliongeza kuwa mara baada ya ripoti hiyo kukabidhiwa kwa Bodi ya Wakurugenzi, haraka uongozi utachukua maamuzi ya kutangaza wachezaji wa kuwaacha na kuwasajili.

“Kesho (leo) kila kinachohusiana na usajili kitajulikana mara baada ya kocha kutukabidhi ripoti ya usajili katika usajili huu wa dirisha dogo.

“Ripoti hiyo ndiyo itakayoamua wachezaji wa kuachwa na kusajili wapya baada ya tetesi nyingi za usajili kusambaa katika vyombo vya habari,” alisema mtoa taarifa huyo.

Simba kwa kupitia Mshauri wa Bodi wa Wakurugenzi ya Simba, Crescentus Magori ilisema: “Ni kweli hatujapata ripoti ya usajili ya kocha hadi hivi sasa, lakini tunatarajia kuipata Jumatatu (juzi) baada ya kutoka Tabora kucheza dhidi ya KMC.

“Baada ya kuipata ripoti hiyo, bodi itakutana kujadili na kuchukua maamuzi ya usajili wa wachezaji wapya ambao kocha amewahitaji pamoja na wa kuachwa.”

SOMA NA HII  KAMA ZALI VILE, TSHABALALA AINGIA ANGA ZA WASAUZI