Home news KUELEKEA KARIAKOO DABI…AUCHO NA BANGALA WATAJWA SIMBA…MORRISON APEWA KAZI MAALUMU…

KUELEKEA KARIAKOO DABI…AUCHO NA BANGALA WATAJWA SIMBA…MORRISON APEWA KAZI MAALUMU…

 


WAKATI joto la pambano la watani Simba na Yanga likiongezeka, nyota wanne wa Yanga wametajwa kuwa mwiba kwa Simba kwenye mchezo huo wa dabi.

Nyota hao ni Feisal, Bangala, Aucho na Mayele ambao wametajwa na mchezaji wa zamani wa Simba, Mtemi Ramadhan akisema watakuwa kikwazo kwenye timu yake hiyo ya zamani kwenye dabi hiyo ya kwanza kwenye Ligi Kuu Tanzania bara msimu huu.

Simba na Yanga zitakutana Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam na mshindi wa mechi hiyo ndiye ataongoza kwenye msimamo ambao sasa Yanga ndio kinara ikiwa na pointi 19 na Simba ni ya pili na pointi 17.

Mtemi amevunja ukimya kuelekea kwenye dabi hiyo, akiwataja wachezaji hao kuwa kikwazo kwa Simba.

“Simba ukabaji wao si mzuri, japo dabi haitabiriki, lakini naamini Bangala, Mayele, Aucho na Feisal watatusumbua sana,” alisema Mtemi.

Alisema Bangala na Aucho wana utulivu wa hali ya juu wakiwa uwanjani, uwa hawana papara na mpira.

“Wametulia wanajua wakati gani watoe pasi na iende wapi, uchezaji wao ni kama wa Lwanga japo tofauti yao ni kwamba Lwanga ana vurugu nyingi uwanjani.

Aucho na Bangala wataisumbua sana Simba, hata Mayele na Feisal, Jumamosi Simba wawe makini nao sana,” alisema.

Alisema kwa timu yake ya Simba, ushindi utaamuliwa na juhudi za wachezaji binafsi.

“Anaweza Morrison (Bernard) akafanya yake, au ikapigwa krosi Kagere (Meddie) akamalizia, naitazamia mechi hiyo kwa Simba,” alisema.

SOMA NA HII  KOCHA AIPELEKA SIMBA NUSU FAINALI AFRIKA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here