Home news KUELEKEA MECHI DHIDI YA YANGA…’TRY AGAIN’ ATOA AHADI YA KIBABE SIMBA..AFICHUA ‘WALIVYOCHEZA...

KUELEKEA MECHI DHIDI YA YANGA…’TRY AGAIN’ ATOA AHADI YA KIBABE SIMBA..AFICHUA ‘WALIVYOCHEZA KAMA PELE’..


MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah Muhene ‘Try Again’, amesema kuwa Yanga ni watoto wadogo kwa Simba na timu yao ipo tayari kuchukua alama tatu, Desemba 11.

Try Again alisema wao wanauchukulia mchezo wao na Yanga kama michezo mingine wanayocheza kwenye ligi nakwamba suala la kupata ushindi kwenye mchezo huo ni zaidi ya asilimia 90.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Try Again alisema kila kitu kimeshakamilika kabla hata hawajasafiri kwenda Zambia na kilichobaki ni kwa upande wa wachezaji kutimiza majukumu yao ndani ya uwanja.

“Yanga kwetu ni timu ya kawaida, hatuna hofu nao hata kidogo, mchezo huo wa dabi tunaona kama mechi nyingine za ligi ambazo huwa tunacheza na timu kutoka nje na Dar es Salaam.

“Mipango imeshakamilika kilichobaki ni kwa wachezaji kutimiza majukumu yao ndani ya uwanja, tunajua kila kitu kuhusu wao na niwahakikishie Wanasimba, Yanga anakwenda kufa,” alisema Try Again.

SOMA NA HII  BAADA YA KUUPATA URAIS YANGA....INJINIA HERSI KUANZA KAZI RASMI LEO...KAMBI YA MAREKANI YATUPWA...SAFARI NI KARATUUU...