Home news KUHUSU ISHU YA CHAMA KUTUA …SIMBA WAAMUA KUANIKA KILA KITU WAZI..BARBARA ATAJWA...

KUHUSU ISHU YA CHAMA KUTUA …SIMBA WAAMUA KUANIKA KILA KITU WAZI..BARBARA ATAJWA KUINJINIA…


UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa, ishu nzima ya usajili wa majembe mapya kwenye kikosi cha timu hiyo akiwemo kiungo Mzambia, Clatous Chama kwa sasa inashughulikiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez.

Chama aliuzwa na Simba miezi minne iliyopita na kujiunga na RS Berkane ya Morocco akisaini mkataba wa miaka mitatu unaotarajiwa kukamilika 2024.

Akizungumza na Spoti Xtra, kuhusu ujio huo wa Chama na mipango ya usajili ya Simba, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, Salim Abdallah ‘Try Again’ alisema: “Kama ambavyo tuliweka wazi kwa Wanasimba katika mkutano wetu mkuu kuwa tumejipanga kufanya usajili mkubwa ambao utatusaidia kutimiza malengo yetu hasa katika mashindano ya kimataifa.

“Kuhusiana na suala la usajili wa Chama, hili ni suala ambalo CEO wetu Barbara Gonzalez analishughulikia na yeye ndiye atakayetoa taarifa zote kuhusiana na masuala ya usajili kwenye kikosi chetu.”

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa RS Berkane anayoichezea Chama, Florent Ibenge, amesema: “Chama ni mchezaji halali wa RS Berkane, bado ana mkataba wa kuendelea kuitumikia timu hii, kuhusu kuomba kuvunja mkataba,

benchi la ufundi na hata viongozi wa Berkane hakuna ambaye anazo taarifa juu ya jambo kama hilo, naamini Chama atasalia hapa.

“Kwa upande wangu kama kocha bado nina mipango na Chama ya kuhakikisha timu yetu inafanya vizuri msimu huu katika mashindano mbalimbali ambayo tunashiriki.”

SOMA NA HII  GOMES - SIJUI LOKOSA YUPO WAPI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here