Home news KUHUSU KUCHEZA DHIDI YA AJIBU KESHO..PABLO APATWA KIGUGUMIZI…ATAJA CHANGAMOTO…

KUHUSU KUCHEZA DHIDI YA AJIBU KESHO..PABLO APATWA KIGUGUMIZI…ATAJA CHANGAMOTO…

 


Kocha wa Simba, Pablo Franco amedai kuwa hayuko tayari kuzungumzia kukutana na nyota wake wa zamani, Ibrahim Ajibu aliyejiunga na Azam FC wakati timu hizo zitakapokutana kesho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kesho.

Kiungo huyo amejiunga na Azam FC jana Desemba 30 baada ya kuvunja mkataba wake na Simba kufuatia mapendekezo ya kocha Franco ya kutaka atolewe kwa mkopo baada ya kukosa nafasi kikosini.

Akizungumza leo, kocha Franco alisema kuwa suala la kukutana na Ajibu kesho haliwazii wala hawezi kulizungumzia kwa sababu hana mamlaka kwa sasa ya kuamua nyota huyo acheze au asicheze katika kikosi cha Azam.

“Suala la Ajibu kucheza litategemeana na kocha wake kwani sio mchezaji wangu kwa sasa. Sijui kama atacheza au hatocheza. Ni mchezaji mzuri lakini changamoto kubwa kwake na wengine tuliowaacha ni nafasi ya kucheza.

Nahitaji kuwa na namba ya wachezaji  ambayo nitaweza kuisimamia mazoezini. Kubwa ninamtakia kila la kheri katika maisha yake mapya na sio yeye tu bali wachezaji wote wanaoondoka,” alisema kocha huyo.

Franco alisema kuwa Ajibu ni mchezaji mzuri ambaye anaamini atafanya vyema na kuisaidia Azam FC.

SOMA NA HII  KISA TFF......SIMBA WAMLA 'KICHWA' KRAMO... ISHU YA NTIBAZONKIZA NI NUSU KWA NUSU...