Home news MDHAMINI WA SIMBA FREDY ‘VUNJA BEI’ ‘ATUA POLISI’…AITAJA YANGA…

MDHAMINI WA SIMBA FREDY ‘VUNJA BEI’ ‘ATUA POLISI’…AITAJA YANGA…


Klabu ya soka ya Tanzania Prisons imeingia mkataba wa kuzalisha vifaa vya michezo na Kampuni ya Vunjabei wenye thamani ya Sh60 milioni.

Mkataba huo uliosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Fredy Ngajiro (Vunjabei) na Kaimu Kamishna wa utawala na usimamizi wa rasilimali watu Jeshi la Magereza Jeremiah Katungu kwenye makao makuu Mkoani hapa.

Aidha licha ya uzinduzi wa jezi pia Vunjabei ameahidi kutoa vifaa vingine katika muda wa mkataba unaendelea ambao ni mwaka mmoja.

Akizungumza kilichomsukuma kufanya ufadhili huo Fredy amesema timu hiyo inajiandaa kuingia kwenye mchezo wake mkubwa wa Disemba 19 dhidi ya Yanga hivyo ni vema wakacheza na Jezi mpya kama ilivyo kwa timu nyingine ikiwa pia ni njia ya kukabiliana na ufinyu wa bajeti unaozikabili timu nyingi nchini.

“Proposal (pendekezo) lilichelewa kuja wakati msimu wa Ligi unaanza lakini kwa uzinduzi wa leo tunatarajia kwenye mchezo wa kesho mtaenda kucheza na Jezi mpya kabla ya mchezo wa Disemba 19” amesema Vunjabei


Aidha Vunjabei amesema imezoeleka kwenye timu za majeshi watu kuziona timu na jezi kama za wanajeshi pekee hivyo kupitia mkataba huo ataifanya jezi hiyo kuwa kwenye viwango vya kibiashara kwa kuitengeneza iweze kuvalika hata na watu wa kawaida.

Mfanyabiashara huyo pia ameahidi kuifanya klabu hiyo kuwa miongoni mwa klabu zitakazojitengenezea uimara katika kuiwezesha kwenye sekta ya vifaa na jezi kwa msimu wa mwaka 2021/2022.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo Kaimu Kamishna wa utawala na usimamizi wa rasilimali watu Jeremiah Katungu ametoa onyo kwa yeyote atakayebainika kuchakachua jezi kwa kutengeneza feki kwa kujipatia maslahi binafsi.

Katungu alimtaka Vunjabei kuongeza wafadhili watakaosaidia kwenye kukabiliana na changamoto zilizopo kwani kufadhili timu hizo ndizo zitasaidia kuibua vipaji kwa wachezaji wa timu ya Taifa huku akiitaka Kampuni ya Sokabet kuendelea na udhamini wake kwenye klabu hiyo.

Naye Mwenyekiti wa timu hiyo Assed Mkwanda amemuomba Vunja Bei kuendelea kudhamini kwenye timu nyingine za michezo kama mpira wa miguu, kikapu na riadha ambazo mara nyingi hukabiliwa na ufinyu wa bajeti.

SOMA NA HII  WAKATI UTAMU WA SOKA UKIZIDI KUONGEZEKA....ODDS ZA UHAKIKA KWA GAME ZA LEO HIZI HAPA..