Home news WAKATI AKIWA KWENYE LISTI YA WANAOACHWA …NTIBAZONKIZA APATA WATETEZI…YANGA YAPEWA ONYO…

WAKATI AKIWA KWENYE LISTI YA WANAOACHWA …NTIBAZONKIZA APATA WATETEZI…YANGA YAPEWA ONYO…


WADAU wa soka nchini wamewashika sikio mabosi wa Yanga na kuwaambia wasifanye makosa ya kumtema Saido Ntibanzonkiza kwani bado ana uwezo mkubwa wa kuisaidia timu hiyo kwenye eneo la ushambuliaji.

Saido tangu mwishoni mwa msimu uliopita hakuwa chaguo la kwanza la kocha Nassredine Nabi lakini kwenye msimu huu kwenye mechi tatu za mwisho kwenye Ligi wakiwa wamecheza mechi saba ameanza kupata nafasi.

Mchezaji na meneja wa zamani Azam Fc, Philip Alando alisema hajawahi kuona Saido akishuka kiwango tangu amekuja Tanzania kujiunga na klabu ya Yanga bali ni nafasi ndio kitu ambacho alikuwa anakosa.

“Ni mchezaji ambaye analeta hamasa kwa wachezaji vijana, tukumbuke huyu ni nahodha wa Burundi na anaendelea kucheza, kuna muda watanzania huwa tuna kasumba ya mchezaji umri mkubwa na tulisema hivyo kwa Kamusoko na hata Saido lakini wamewaumbua watu wengi baada ya kufanya makubwa zaidi hata ya wachezaji wenye umri mdogo,” alisema Alando.

Naye mshambuliaji wa zamani Yanga, Hery Morris alisema;”Kiukweli huyu ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa na anaweza kutoa matokeo kwa muda wowote ule,mpaka sasa kwa kiwango fulani ameziba pengo la Yacouba (Sogne) lakini kila mchezaji ana utofauti wake kwenye uchezaji kwahiyo kwa nafasi zao wanacheza vizuri.”

Mshambuliaji huyo alianza kurejea katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting akiingia akitokea benchi, mchezo dhidi ya Namungo akifunga bao la kusawazisha kwenye sare 1-1 na mchezo wa mwisho ni dhidi ya Mbeya Kwanza walioshinda 2-0 huku akifunga bao la kwanza kwa mpira wa adhabu na bao la pili likifungwa na Fiston mayele.

SOMA NA HII  KAMA ULIKUWA HUJUI...HAYA HAPA MAAJABU YA CHAMA NDANI YA SIMBA TOKA AMERUDI BONGO..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here