CLATOUS Chota Chama, nyota wa Simba Sc amesema kuwa ni furaha kubwa kwake kurejea ndani ya timu hiyo.
Chama aliibuka ndani ya RS Berkane msimu wa 2021/22 akitokea Klabu ya Simba na amerejea tena nyumbani.
Ni usajili wa kwanza katika dirisha dogo ambapo jana hakuwa sehemu ya mchezo dhidi ya Mbeya City ambao wameupooteza kwa kichapo cha goli moja bila kwenye Uwanja wa Sokoine.
Nyota huyo amesema:โNafurahi kurejea Simba, nimerudi nyumbani na nina amini kwamba tutapambana kuchukua makombe,โ.