Home news BAADA YA CHAMA KURUDI SIMBA JANA…YANGA KUJIBU MAPIGO LEO…WADAI NCHI ITASIMAMA..NI MSUVA..?

BAADA YA CHAMA KURUDI SIMBA JANA…YANGA KUJIBU MAPIGO LEO…WADAI NCHI ITASIMAMA..NI MSUVA..?


Klabu ya Young Africans imeahidi kumtangaza mchezaji wa kimataifa aliyesajiliwa klabuni hapo katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo ambacho kitafungwa rasmi leo Jumamosi (Januari 15).

Young Afruicans imetamba kumtangaza mchezji huyo, kupitia kwa Msemaji wao Haji Sunday Manara, alipozungumza na Waandishi wa Habari mjini Tanga mapema jana Ijumaa (Januari 14).

Manara amesema kabla ya Dirisha Dogo la Usajili halijafungwa kesho Jumamosi (Januari 15), klabu hiyo itamtangaza mchezaji wa kimataifa ambaye hakuwa tayari kumtaja jina lake.

Amewata Mashabiki na Wanachama wa Young Africans kuwa tayari kumpokea mchezaji huyo ambaye anaaminiwa ataongeza chachu ya kusaka taji la Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2021/22.

“Kabla Dirisha halijafungwa kesho {leo}Jumamosi, tutamtangaza mchezaji wa kimataifa, Mashabiki na Wanachama mjiandae kumpokea mchezaji huyo ambaye tunaamini ataongeza kitu kwenye kikosi chetu kinachowania ubingwa msimu huu kwa nguvu zote.” 

Amesema Manara. Katika kipindi cha Dirisha Dogo la usajili 2021/22, Young Africans tayari imeshawasajili wachezaji kadhaa akiwepo Denis Nkane, Aboutwalib Mshery, Crispin Ngushi, Salum Aboubakar ‘Sure Boy na Ibrahim Bacca.

Hata hivyo duru za kuaminika zinasema kuwa huenda Yanga leo wakatangaza kumrudisha kikosini mshambuliaji wake wa zamani Simon Msuva ambaye kwa siku za hivi karibuni anaripotiwa kutokuwa na timu yake ya Morocco.

Msuva ambaye yupo nchini toka mwaka jana kwa kile kinachosemekana kuigomea Waydad Casablanca kwa kutomlipa stahiki zake mbalimbali.

Itakumbukwa kuwa Yanga walimuuza Msuva nchini Morocco misimu kadhaa nyuma , ambapo toka aende huko amekuwa na wakati mzuri mpaka kujiunga na timu kubwa kwenye taifa hilo la kaskazini mwa Afrika.

Pia inasemekana huenda akawa ni Chico Ushindi kutoka TP Mazembe, ambaye kwa muda mrefu sana Yanga wamekuwa wakihitaji huduma yake, kabla ya hivi karibuni kutoka taarifa kuwa Yanga imeshindwa kulipa gharama za kumchukua kwa mkopo.

SOMA NA HII  MGUNDA AWEKA MAMBO HADHARANI SAKATA LA ROBERTINHO NA PHIRI SIO POA, ISHU IKO HIVI