Home news BAADA YA KUICHEZEA YANGA KWA MARA YA KWANZA..CHICO AIKISA KICHWA..KISHA AKANENA HAYA...

BAADA YA KUICHEZEA YANGA KWA MARA YA KWANZA..CHICO AIKISA KICHWA..KISHA AKANENA HAYA MAZITO…


WINGA mpya wa Yanga, Chico Ushindi ameangalia kikosi hicho akatamka; “Tunabeba.”

Staa huyo aliyesajiliwa dirisha dogo akitokea TP Mazembe ya DR Congo, juzi jioni alicheza mechi yake ya kwanza Jijini Arusha timu  dhidi ya Mbuni FC.

Chico amesema kwa jinsi alivyoona ushindani kwenye mechi dhidi ya Coastal Union na hali ilivyo kambini na mazoezini ana uhakika Yanga itafanya vizuri msimu huu na ni aina ya timu zenye ushindani anaotaka yeye.

Alisema kwa timu alizoona kwenye vyanzo mbalimbali mpaka sasa anadhani Yanga ina nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwa vile wana wachezaji wenye uwezo na hamu ya mafanikio.

“Ushindani ni mkubwa sana, sioni jinsi tunaweza kukosa ubingwa msimu huu. Sijaona timu zote lakini kwa ninachokijua mpaka sasa naona nafasi yetu ni kubwa,” aliongeza mchezaji huyo aliyekiri anatagemea ushindani mkubwa wa namba ndani ya kikosi.

USHINDANI

Chico anakuwa ni winga wa saba ndani ya kikosi cha Nabi, akipambana na Deus Kaseke, Dickson Ambundo, Denis Nkane, Jesus Moloko, Farid Mussa, Said Ntibazonkiza na Yacouba Sogne.

Kwenye idadi hiyo ya mawinga Nabi amekuwa akiwatumia mara kwa mara Moloko, Ntibazonkiza na Farid, hivyo ujio wa winga huyo kutoka Mazembe unatoa nafasi ya mchezaji mmoja kupungua kikosini.

Yacouba yupo nje ya uwanja kwa muda sasa kutokana na kusumbuliwa na jeraha la goti na nafasi yake Nabi amekuwa akimpanga Ntibazonkiza ambaye ameonekana kuwa vizuri akifunga mabao manne hadi sasa katika Ligi Kuu na kutoa pasi za mabao kwa wenzake.

Ntibazonkiza amekuwa tegemeo Yanga kwa mapigo ya mipira iliyokufa, akifunga bao kwa frii-kiki ya moja kwa moja na penalti, huku pia akipiga kona na adhabu ndogo zote na kutokana na uwezo wake wa kuchezesha timu na kutengeneza nafasi za kufunga, ni wazi nyota huyo wa Burundi ana uhakika wa namba kikosini.

Farid, hajafunga bao lakini amehusika katika mabao kadhaa muhimu ya Yanga msimu huu, likiwamo la ushindi wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba lililofungwa na Fiston Mayele Septemba 25, 2021 kwenye Uwanja wa Mkapa na la juzi alilomtengea Saido na kuwapa kujiamini Yanga wakishinda 2-0 dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Kwa ushindi huo Yanga walipewa Sh70 milioni.

SOMA NA HII  WYDAD WAANZA KUIFANYIA SIMBA FIGISU....RAIS WAO AJIAPIZA KUMALIZA KAZI MAPEMA TU...

Jesus Moloko amehusika moja kwa moja katika mabao nane kwenye michuano yote, akifunga mabao manne, ametoa asisti mbili na kusababisha penalti mbili, hivyo ni kati ya watu muhimu zaidi katika ushambuliaji wa Yanga huku akiwa mchapakazi anayesaidia sana ulinzi kwani hushuka mara kwa mara wanaposhambuliwa.

Yanga imemsajili staa wa Biashara United, Nkane ambaye alikuwa na mabao mawili katika timu yake ya zamani na ametua kwa kishindo Yanga akifunga bao moja katika Kombe la Mapinduzi.

Ujio wa ushindi unaweza kuwatikisa zaidi Ambundo, ambaye amerejea kutokea kuwa majeruhi na Kaseke ambaye msimu uliopita alitengeneza pacha ya kutisha na Yacouba, lakini msimu huu amekosa nafasi ya kucheza mara mara.

Akizungumza Ushindi alisema amekuja Yanga baada ya kuzungumza na Kocha Nabi Mohamed ambaye alimweleza anachotaka aje kufanya ambacho ni kuongeza kasi ya upatikanaji wa mabao.

“Naweza kufunga na kutengeneza mabao kwa wengine, naamini tukishirikiana mambo yatakuwa rahisi,” alisema Ushindi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here