Home news BAADA YA KUONA VIWANGO VYA SHIBOUB NA MOUKORO..MATOLA ASHINDWA KUJIZUIA ..ADAI NI...

BAADA YA KUONA VIWANGO VYA SHIBOUB NA MOUKORO..MATOLA ASHINDWA KUJIZUIA ..ADAI NI VUGUMU…


WACHEZAJI Sharaf Shiboub na Cheick Moukoro walio kwa majaribio na timu ya Simba mjini Zanzibar wameelezwa kuanza vyema majaribio yao katika timu hiyo.

Wachezaji hao jana walikuwa kwenye kikosi cha Simba kilichopata ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya Selem View ya Pemba katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi, Uwanja wa Amani, mjini Zanzibar, ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Kocha Msaidizi wa Simba, Suleiman Matola alisema ameona uwezo wa wachezaji hao na wameanza vyema, lakini ni vigumu kwa mechi moja kuweza kuwatolea uamuzi ingawa wameonesha uwezo mzuri uwanjani.

‘’Tutaendelea kuwaona na mechi nyingine, lakini wameonesha uwezo mkubwa kwa mechi ya leo,’’amesema Matola.

Katika mchezo huo mabao ya Simba yalifungwa na Msenegal, Pape Ousmane Sakho dakika ya 25 na Mzambia, Rally Bwalya dakika ya 53.

SOMA NA HII  BIGIRIMANA BADO SANA YANGA....ISHU YAKE YA KURUDI UPYA IKO HIVI....