Home news KISA NKANE, MSHERY NA NGUSHI..NABI AFANYA MAAMUZI MAGUMU YANGA..MWAKALEBELA KAMA KAWA…

KISA NKANE, MSHERY NA NGUSHI..NABI AFANYA MAAMUZI MAGUMU YANGA..MWAKALEBELA KAMA KAWA…


KOCHA Mkuu wa Yanga, raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi, amenogewa na ubora wa wachezaji wazawa aliowasajili katika dirisha dogo huku akipanga kusimamisha usajili wa nyota wa kigeni katika msimu ujao.

Baadhi ya wachezaji wazawa waliosajiliwa katika dirisha dogo ni Aboutwalib Mshery, Denis Nkane, Chrispin Ngushi na Salum Aboubakari ‘Sure Boy’.

Wachezaji hao wote wamesajiliwa kwa mapendekezo ya Nabi baada ya kuwaona katika michezo ya Ligi Kuu Bara mara walipokutana kucheza na timu zao za zamani kabla ya kutua Yanga.

Mmoja wa mabosi wa timu hiyo, amesema kuwa kocha huyo hafikirii kuongeza mchezaji mwingine wa kigeni katika usajili wa msimu ujao baada ya kuvutiwa na vipaji vya wachezaji wa hapa nchini.

Bosi huyo alisema kuwa kikubwa alichopanga ni kusajili wachezaji wazawa vijana wenye uwezo mkubwa kama waliokuwa nao Ngushi, Nkane na Mshery.

Aliongeza kuwa kikubwa anataka kuona timu hiyo ikiundwa na wachezaji wengi wazawa wenye umri mdogo watakaocheza kwa muda mrefu katika kikosi chake.

“Kama ikitokea kocha atasajili wachezaji wa kigeni, basi ni mmoja kwani mipango yake katika usajili wa msimu ujao ni kusajili wachezaji wazawa pekee katika timu.

“Kipaumbele hicho anakitoa kwa wazawa baada ya kuvutiwa na baadhi ya wachezaji ambao amewasajili katika dirisha dogo la msimu akiwemo Mshery, Nkane na Ngushi.

“Pia upo uwezekano wa kupunguza wachezaji wa kigeni, na kikubwa anataka kubaki na nane pekee ambao wanaanza katika kikosi cha kwanza kutokana na kanuni za TFF zilizopo za kutumia wachezaji nane katika kikosi cha kwanza,” alisema bosi huyo.

Alipotafutwa Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela kuzungumzia hilo alisema: “Muda wa usajili mkubwa bado haujafikia, kingine masuala ya usajili yote yapo kwa kocha wetu.”

SOMA NA HII  BAADA YA KUPEWA MECHI YA KWANZA....GAMONDI ASHINDWA KUJIZUI KUHUSU GUEDE....