Home news KUHUSU MECHI DHIDI YA YANGA KUCHEZWA MANUNGU AU LAH..MTIBWA WATOA UFAFANUZI HUU...

KUHUSU MECHI DHIDI YA YANGA KUCHEZWA MANUNGU AU LAH..MTIBWA WATOA UFAFANUZI HUU MPYA…


OFISA Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru ameweka wazi kwamba hawafikirii kuacha kuutumia Uwanja wa Manungu kwa wakati huu kwenye mechi za Ligi Kuu Bara ambazo zipo mbele yao ikiwa ni pamoja na ile dhidi ya Yanga.

Akizungumza na Gazeti la Championi , Kifaru alisema kuwa uwekezaji ambao wameufanya unawapa nguvu ya kutumia uwanja wao bora ambao upo kwenye viunga vya miwa Morogoro.

“Sisi tumefanya uwekezaji bora na imara na mashabiki wa Mtibwa Sugar wanatambua kwamba tupo imara na baada ya Simba kucheza Uwanja wa Manungu hata Yanga nao tutawaleta hapa.

“Hatufikirii kuondoka hapa zaidi ya kuendelea kuuboresha uwanja wetu, hatujiendeshi kwa kutegemea mapato ya uwanjani bali uwezo upo na tupo imara,” alisema.

Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 13 ikiwa imekusanya pointi 12 baada ya kucheza mechi 13 na safu yake ya ushambuliaji imefunga mabao saba. Walipocheza na Simba uwanjani hapo walitoshana nguvu ya bila kufungana.

SOMA NA HII  BAADA YA KUMALIZANA NA WATUNISIA... MKAKATI WA YANGA 'KUIPELEKEA MOTO' MAZEMBE UKO HIVI...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here