Home news PABLO AAMUA LIWALO NA LIWE SIMBA…AWAPIGA CHINI SHIBOUB NA MOUKORO…’TRY AGAIN’ ATOA...

PABLO AAMUA LIWALO NA LIWE SIMBA…AWAPIGA CHINI SHIBOUB NA MOUKORO…’TRY AGAIN’ ATOA KAULI…


Kocha wa Simba, Pablo Franco amewakataa wachezaji wa majaribio, Sharaf Shiboub wa Sudan na Cheick Moukoro kutoka Ivory Coast kutokana na kutoridhishwa na viwango vyao.

Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ aliweka wazi kuwa hata kama nyota hao wangesajiliwa wasingekuwa kwa ajili ya msimu huu.

Wakati Pablo akiwakataa nyota hao wawili waliocheza mchezo wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Selem View, imeelezwa kuwa mchezaji kutoka Nigeria, Udoh Etop, ambaye alianza mazoezi juzi usiku kabla ya mechi ya dhidi ya Mlandege FC kupewa nafasi zaidi ya kuonyesha uwezo wake.

Hata hivyo, habari kutoka ndani ya timu hizo zinadai kuwa kocha Pablo Franco bado hajaridhishwa na kiwango cha wachezaji hao wawili Shiboub na Moukoro, huku Etop akiendelea kumpa nafasi ya kumwangalia zaidi kwani alichelewa kuanza na wenzake.

Habari za ndani ya klabu hiyo zilieleza pia kuwa Pablo amewaambia mabosi wake kusitisha mpango wa kuwaleta wachezaji kwa ajili ya majaribio na anachokitaka ni wachezaji watakaosajiliwa moja kwa moja na kuanza kucheza.

Kuhusu hilo Pablo, awali alisema: “Nahitaji muda zaidi wa kuwaangalia maana wamekuja kwa ajili ya majaribio, hivyo ngoja tusubiri muda ufike.”

Akizingumza  jana, Try Again alifafanua juu ya uwepo wa wachezaji hao na nini wanachokitarajia kutoka kwao mara baada ya kocha wao kutoa uamuzi wake.

“Wachezaji hawa tunawaletea wenyewe kwa gharama zetu kuanzia tiketi na kila kitu, ni kweli tunatumia gharama, lakini si tatizo kwetu kwani Simba ni klabu inayojiweza kwenye uchumi, hivyo hatuoni hasara kwa lolote litakalotokea.

“Hadi sasa kocha bado hajatueleza lolote kuhusu wachezaji hao kama ameridhishwa ama hajaridhishwa na viwango vyao. Hata kama atasema tuwasajili basi tutafanya hivyo, ila hawatakuwa miongoni mwa wachezaji watakaocheza mashindano yoyote ya msimu huu, ambayo tunashiriki bali watakuwa ni kwa ajili ya msimu ujao.

“Tutawasajili lakini tutawapeleka kwenye timu zingine kwa mkopo ili waendelee kucheza huko kwa ajili ya kulinda viwango vyao. Hivyo kwa ufupi maamuzi ya kocha ndiyo tutakayoyafanyia kazi juu ya wachezaji hawa,” alisema Try Again

SOMA NA HII  ROBERTINHO APATA MBADALA WA INONGA

Hata hivyo, kuna kuna taarifa kwamba nyota wao wa zamani, Clatous Chama atajiunga na Simba muda wowote kujiunga na kikosi hicho, huku ikidaiwa kwamba mshambuliaji Moses Phiri wa Zambia anayedaiwa pia kujiunga na timu hiyo msimu ujao.

Simba imebakiza nafasi moja ya kusajili mchezaji wa kimataifa, hivyo Moukoro, Shiboub, Etop na Phiri watawania nafasi moja kama watataka kuwatumia katika msimu huu.