Home news WAKATI AKISEMEKANA KUSAINI YANGA..WAKALA WA MOSES PHIRI AMALIZA UTATA…AIBUKA NA HILI..

WAKATI AKISEMEKANA KUSAINI YANGA..WAKALA WA MOSES PHIRI AMALIZA UTATA…AIBUKA NA HILI..


Wakala wa Kiungo Mshambuliaji kutoka Zambia Moses Phiri amethibitisha taarifa za kutafutwa na Viongozi wa Young Africans ili kuangalia uwezekano wa kumsajili mchezaji wake.

Phili anatajwa kuwaniwa na klabu za Simba SC na Young Africans zote za Dar es salaam-Tanzania, katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la Usajili.

Wakala wa Kiungo huyo amesema Viongozi wa Young Africans wamemtafuta na yeye kama mtu wa karibu na mchezaji huyo aliona umuhimu wa Phili kuondoka Zambia, lakini Uongozi wa Zanaco umeweka ngumu.

Amesema Uongozi wa Zanaco FC hauko tayari kumuachia Phiri katika kipindi hiki ambacho timu yao inajiandaa na Mshike Mshike wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya Makundi.

“Young Africans wamenitafuta kuhusu Phiri lakini Uongozi wa Zanaco FC umeweka msimamo wa kutaka kumtumia kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho itakayoendelea mwezi Februari.”

“Suala la kupokelewa kwa ofa litafunguliwa rasmi mwishoni mwa msimu huu, kwa sasa ni ngumu kwa mchezaji huyu kuondoka hapa Zambia, japo mimi kama wakala wake nilitaka kuona anaondoka na kucheza soka Tanzania.” amesema wakala wa Phiri.

Klabu za Simba SC na Young Africans zimedhamiria kuviboresha vikosi vyao katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la Usajili, ili kukoleza makali ya kufukuzia ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu 2021/22.

SOMA NA HII  NAMUNGO YAPANIA KUFANYA VIZURI KIMATAIFA