Home news WAKATI DIARRA AKIWA NJIANI KURUDI YANGA…MSHERY AKUNA KICHWA WEE..KISHA KWA KUJIAMINI AFUNGUKA...

WAKATI DIARRA AKIWA NJIANI KURUDI YANGA…MSHERY AKUNA KICHWA WEE..KISHA KWA KUJIAMINI AFUNGUKA HAYA…


KIPA wa Yanga, Aboutwalib Mshery amesema kuwa atatumia uwezo wa kipa mwenzake, Djigui Diarra katika kujifunza mambo mbalimbali ndani ya timu hiyo akiamini atamsaidia kufikia uwezo wa kimataifa.

Mshery ameongeza kuwa kwake wala hahofii nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza mara baada ya kurejea kwa nyota huyo.

Diarra anarejea ndani ya Yanga baada ya kukosekana kwa muda kutokana na kwenda kulitumikia taifa lake la Mali kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) inayoendelea nchini Cameroon. Mali waliondolewa hatua ya 16 bora.

Mshery alisajiliwa maalum na Yanga kwa ajili ya kuziba nafasi ya Diarra akitokea Mtibwa Sugar ambapo kwa sasa kutakuwa na ushindani kati ya makipa hao.

Akizungumza na  Gazeti la Championi , Mshery alisema kuwa anaamini uwepo wa Diarra utakuwa chachu kwake katika kujifunza mambo mengi mbalimbali kutokana na uwezo wake huku akiwa hana hofu juu ya kucheza kwa sababu ya uwepo wa michezo mingi kikosini humo.

“Diarra ni kipa mkubwa, ana uzoefu katika soka la Afrika hivyo natarajia kujifunza mambo mengi kutoka kwake, hivyo kuwa naye tu katika timu moja inatosha mimi kupata baadhi ya vitu ambavyo vitakuwa na msaada mkubwa kwangu.

“Kuhusu kupata nafasi mbele yake, naamini kocha ndiyo anafahamu zaidi lakini kwa upande wangu naamini kuna michezo mingi sana ya ligi kuu na Kombe la Shirikisho, hivyo naamini nafasi ya kucheza nitapata,” alisema kipa huyo.

SOMA NA HII  MGUNDA ATAJWA ISHU YA DOGO WA SIMBA KUFUNGA JUZI...ISHU NZIMA ILIKUWA HIVI...