Home news BAADA YA KUTULIA….DEWJI ATOA TAMKO KUHUSU MUSTAKABLI WA MORRISON…ATAKA APEWE MASHARTI MAGUMU…

BAADA YA KUTULIA….DEWJI ATOA TAMKO KUHUSU MUSTAKABLI WA MORRISON…ATAKA APEWE MASHARTI MAGUMU…


WAKATI mashabiki wa Yanga wakiwa wamegawanyika juu ya taarifa za awali za mabosi wao kuanza kumzengea winga wa Simba, Bernard Morrison, Mfadhili wa zamani na mwanachama wa Simba, Azim Dewji ameamua kumzuia rasmi Simba. 

Morrison, mfungaji wa bao la kusawazisha la Simba dhidi ya USGN ya Niger katika mechi ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, alisimamishwa na klabu yake kwa utovu wa nidhamu kabla ya kurejea na kuikoa timu isiaibike nchini Niger, amekuwa akihusishwa na Yanga wakati mkataba wake Msimbazi ukielekea kuisha.

Hata hivyo, bilionea huyo wa zamani wa Simba, Azim amekiangalia kiwango cha Mghana huyo na kukiri kukoshwa naye na kusema anatamani mkataba mpya wa kumfanya abaki ila akitaka apewe masharti maalumu.

Azim alisema masharti hayo ni kutafutiwa mtaalamu maalumu wa masuala ya kisaikolojia ambaye atasaidia kumuweka sawa kiakili mshambuliaji huyo lakini awekewe vifungu katika mkataba wake vitakavyombana na kumzuia kujihusisha na vitendo vya utovu wa nidhamu.

Bilionea huyo enzi akiifadhili Simba aliiwezesha kufika Fainali ya Kombe la CAF 1993 na kupoteza 2-0 na Stella Abidjan, alisema Morrison ni mchezaji mzuri ambaye kila timu hapa nchini inatamani kuwa naye lakini kinachomuangusha mchezaji huyo kutoka Ghana ni changamoto ya kinidhamu.

“Morrison ni mchezaji mzuri na kama unavyoona juzi ametufungia bao muhimu ugenini dhidi ya timu ya Niger(US Gendarmerie) ambalo limetupatia pointi na kutufanya tuongoze kundi jambo ambalo ni zuri,” alisema Azim na kuongeza;

“Napenda kuona akiendelea kuichezea Simba kwani ana kipaji na uwezo mkubwa ingawa lazima itafutwe njia ya kumsaidia nayo ni kupatiwa mtaalam wa kisaikolojia ambaye atamuweka sawa na kumfanya atulie na awe na nidhamu ya hali ya juu. Akitulia anatoa mchango mkubwa sana kwa timu.”

Azim alisema hana shaka na kiwango na kipaji cha Morrison lakini masuala ya utovu wa nidhamu yatamrudisha nyuma hivyo mchezaji huyo anayemudu vyema kucheza nafasi ya winga na mshambuliaji wa kati anapaswa kubadilika na kuwa na tabia njema.

SOMA NA HII  KUHUSU WANAOM'BEZA KUWA HATAIWEZA NAFASI YA CHAMA...BWALYA AWAJIBU HIVI

Kauli hiyo ya Azim ni kama inafuta ila aliyoitoa mwaka jana pale alipolishauri Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kumrudisha mchezaji huyo nchini Ghana baada ya kuziingiza kwenye mgogoro wa kiusajili, Simba na Yanga.

“Kwa upande wangu naona ni kitu chepesi tu. TFF wamrudishe huyo mchezaji kwa sababu mbili muhimu. Huyu mchezaji akichukua maamuzi ya kuchezea Yanga hawawezi kumchezesha na kwa ajili watakuwa hamuamini. Na akija upande wa Simba huyu kijana hana nidhamu sasa ataanza kuharibu wachezaji wengine,” alinukuliwa Azim.

Hivi karibuni, Morrison alisimamishwa na Simba kwa muda usiojulikana baada ya kudaiwa kuondoka kambini bila ruhusa ingawa baadaye alirudishwa kundini baada ya klabu hiyo kusema kuwa aliandika barua ya kuomba msamaha. kusawazisha ugenini dhidi ya Gendarmerie Nationale, Jumapili iliyopita.