Home news KUHUSU NABI KUONGEZWA MKATABA YANGA..SENZO AFUNGUKA HAYA…ADAI WAPO VITANI KWANZA..

KUHUSU NABI KUONGEZWA MKATABA YANGA..SENZO AFUNGUKA HAYA…ADAI WAPO VITANI KWANZA..


MTENDAJI Mkuu wa Yanga, Senzo Mazingisa amesema kuwa wanatambua kazi bora ya Nasreddine Nabi na ishu yake ni kama imeisha, kwani watamuongezea mkataba wa miaka miwili au mitatu haraka kabla ya ligi kumalizika, hivyo mashabiki watulize mzuka.

Senzo ambaye ni Msauzi, alisema Yanga inafahamu Nabi anaweza kuwa na ofa nyingi, lakini jambo zuri kwao katika mazungumzo na kocha wao huyo bado anataka kubaki Yanga.

“Kocha bado ana kazi yake hapa anaendelea nayo jambo zuri tulishazungumza naye lakini chaguo lake la kwanza ni kubaki hapa kwa muda mrefu zaidi na tutamalizana naye,” alisema Senzo jana ofisini kwake katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

“Kwa sasa tupo vitani jambo zuri hata Nabi amekuwa akizungumza nasi kuhusu hilo atakapopata muda, kwani akili yake ipo sana katika kuandaa timu kushinda, watu wasichofahamu Nabi ni kocha anayependa mafanikio ya kazi. Hivyo muda mwingi anataka afikirie kazi yake nasi tunaheshimu hilo,” alisema Senzo.

Mkataba wa sasa wa Nabi na Yanga ulikuwa wa mwaka mmoja na utamalizika Juni mwaka huu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Yanga, Dominic Albinius alisema wameshauriana na Nabi asaini mkataba wa miaka miwili wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi ingawa hakutaja masilahi yake.

Albinius alisema wamependekeza mkataba huo usainiwe haraka kutokana na uhaba wa makocha bora kama Nabi katika soko la makocha kwa sasa.

“Unajua zipo timu zinatamani kuwa na kocha kama huyu hata humu ndani zipo, sasa sisi kama Kamati tumewaambia uongozi wa juu uchukue hatua kwani hata kocha amekubali,” alisema Albinius na kuongeza;

“Ni vigumu sana kupata makocha kama hawa na sisi kama Yanga hatutaki kufanya makosa kama hayo na tumekuwa tukiongea naye mambo haya muda mrefu na kama mnavyoona amekuwa akifanya usajili wa muda mrefu katika timu hii kwa kuwa anajua kila kitu juu ya malengo ya klabu yetu.”

Msikie Nabi

Nabi amesema kwa sasa anaendelea na kazi na anatamani kubaki zaidi Yanga kutokana na mapenzi ya mashabiki na ushirikiano anaoupata kutoka kwa uongozi wa Yanga kuanzia tajiri wao Ghalib Said na Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla.

SOMA NA HII  RAGE - LIGI KUU IMESHAKUWA NGUMU KWA SIMBA...YANGA WANAVYOCHEZA HUONI LINI WATAPOTEZA..

“Nafurahi kuwa hapa nafikiri hayo mambo ya mkataba ni vyema wakayaongelea sana uongozi,binafsi nafurahi kuwa sehemu ya Yanga najiona niko salama nikiwatumikia mashabiki wakarimu na wanaoipenda timu yao, ila hasa ninavyopewa ushirikiano na mdhamini wetu Ghalib na mwenyekiti.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here