Home news NABI AWAPANGIA BIASHARA FULL MKOKO..KOCHA WA BIASHARA AMTUNUSHIA MISULI…

NABI AWAPANGIA BIASHARA FULL MKOKO..KOCHA WA BIASHARA AMTUNUSHIA MISULI…


YANGA watashuka dimbani leo Jumanne kucheza na Biashara United kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora ndani ya Dimba la Mkapa, Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 usiku.

Mchezo huo wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports, utaamua nani anakwenda hatua ya robo fainali.

Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi, baada ya kufanya maandalizi kwa takribani wiki moja, leo amepanga kuweka kikosi chake cha ushindi kutokana na umuhimu wa mchezo huo.

Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Thabity Kandoro, ameliambia Spoti Xtra kuwa: “Mchezo wetu wa kesho (leo) utakuwa na umuhimu mkubwa sana wa kupata matokeo ya ushindi kwa sababu tunahitaji kuvuka hapa na kwenda hatua inayofuata.

“Kocha Nabi nilipozungumza naye aliweka wazi kuwa anataka kuweka mkoko wa maana kwenye mechi hiyo kwani kwa vyovyote anahitaji kushinda na kusonga mbele zaidi hadi fainali na kuwa mabingwa.”

Kwa upande wa Biashara United, Kocha Mkuu, Vivier Bahati, alisema: “Tunamshukuru Mungu tumemaliza maandalizi kuelekea mchezo wetu wa kesho (leo) dhidi ya Yanga.

“Wachezaji wote wapo fiti, tutahakikisha tunapambana na kupata matokeo mazuri kwa ajili ya kuvuka katika hatuainayofuata kwani mipango yetu ni kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya kimataifa msimu ujao.”

Yanga na Biashata United zinakwenda kukutana ikiwa imepita takribani miezi miwili, mara ya mwisho zilikutana Desemba 26, 2021 ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara uliomalizika kwa Yanga kushinda 2-1.

SOMA NA HII  KILICHO NYUMA YA KUSIMAMISHWA KWA NYOTA WATATU AZAM FC HIKI HAPA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here