Home news WAKATI SIMBA WAKINYATIA SAINI ZA KINA MWAMNYETO…YANGA WAIBUKA NA KUTOA KAULI HII..

WAKATI SIMBA WAKINYATIA SAINI ZA KINA MWAMNYETO…YANGA WAIBUKA NA KUTOA KAULI HII..


UONGOZI wa Yanga, umezima tetesi za kuondoka baadhi ya wachezaji ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu na kuweka mazingira ya kuwapa mikataba mirefu.

Chanzo cha ndani kutoka Yanga kimesema kuwa: “Ndani ya Yanga hakuna atakayeondoka tena, kwa sababu inataka kujenga timu yenye kikosi kipana, wote ambao mikataba yao ipo ukingoni itaongezwa.”

Championi lilimtafuta Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Thabity Kandoro ili kujua ukweli wa taarifa hizi ambapo alisema: “Kwa kawaida timu inayotengeneza kikosi bora haiwezi kuacha mchezaji holela.

“Kwa sababu kwa kufanya hivyo inakuwa ni sawa na kurudi nyuma baada ya kwenda mbele, Yanga itawapa mikataba mipya wachezaji wote ambao mikataba yao ipo ukingoni, hakuna atakayeondoka.”

Baadhi ya wachezaji wa Yanga ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu ni nahodha Bakari Mwamnyeto, Kibwana Shomari, Saidi Ntibazonkiza, Yacouba Songne, Deus Kaseke na Abdallah Shaibu ‘Ninja’.

SOMA NA HII  MAPINDUZI BALAMA, DICKSON JOB KAMILI GADO KWA KAZI YANGA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here