Home news WAKATI SIMBA WAKISIMAMIA UKUCHA KWENYE JEZI ZAO…YANGA WAKUBALI KUSHUKA…MANARA IBUKA NA KAULI...

WAKATI SIMBA WAKISIMAMIA UKUCHA KWENYE JEZI ZAO…YANGA WAKUBALI KUSHUKA…MANARA IBUKA NA KAULI HII…


KLABU ya Yanga imepunguza bei ya jezi zake ili kuwapa nafasi mashabiki wake kununua jezi za timu yao kwa bei nafuu zaidi.

Kaui hiyo imetolewa jana Jumatatu, Februari 21, 2022 na mhamasishaji wa klabu hiyo, Haji Manara wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar.

“Tumetoa punguzo maalum la jezi kwa jumla na rejareja, rejareja sasa ni Tsh. 30,000 jumla ni Tsh. 22, 000, tunataka kuongeza hamasa kwenye viwanja vya mpira tunataka watu ‘wa-focus’ na furaha ndiyo maana tumewaletea punguzo.

“Kwa statistics (takwimu), Yanga imeuza jezi mara tano ya idadi ya jezi zilizouzwa na vilabu vyote vya ligi kuu kwa msimu huu,” amesema Manara.

Wakati Yanga wakishusha beo jezi zao, Wenzao Simba SC wameendelea kutamba na bei ile ile ya awali, huku wakizidi kuzindua jezi mbalimbali za mashindano wanayoshiriki.

Kuhusu mchezo wao ujao dhidi ya Mtibwa Sugar, Manara amesema Kikosi cha Yanga kipo tayari kuwavaa Mtibwa na wanaamini watashinda mechi hiyo mapema kwa kuwa maandalizi yako vizuri kuanzia benchi la ufundi na wachezaji.

SOMA NA HII  BAADA YA KUTEMWA YANGA BILA KUTARAJIA....'NINJA' AKUMBUKA ALIYOAMBIWA NA ZLATAN...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here