Home news YANGA WAKIZUBAA TU…MWAMNYETO HUYOOO MSIMBAZI…VIGOGO SIMBA KUKUTANA NA WAKALA WAKE LEO..

YANGA WAKIZUBAA TU…MWAMNYETO HUYOOO MSIMBAZI…VIGOGO SIMBA KUKUTANA NA WAKALA WAKE LEO..


Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC wanahusishwa na mpango wa kuanza mazungumzo na Nahodha na Beki kati wa klabu ya Young Africans, Bakar Nondo Mwamnyeto.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zimethibitisha kuwa Uongozi umedhamiria kuipata saini yake huku ikifahamika kuwa leo Jumatano (Februari 02), huenda ukafanya mazungumzi na meneja wa mchezaji huyo Kasa Musa.

Simba SC pia bado wamemng’ang’aninia kiraka wa Yanga SC Kibwana Shomari ambao wote kandarasi zao zinaisha mwisho wa msimu huu.

Hata hivyo Klabu ya Simba SC haijazungumza lolote kuhusu mpango huo kwa wachezaji wote wawili, zaidi ya kuendelea kuzungumza kama Tetesi katika mitandao ya kijamii.

SOMA NA HII  MMISRI KUAMUA MECHI YA HOROYA vs SIMBA...KWA KUTOA KADI TU ..HAJAMBO KWA KWELI...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here