Home Azam FC AZAM FC WAIFUATA NAMUNGO KIBABE…ZAKA ZAKAZI AIBUKA NA HILI JIPYA…

AZAM FC WAIFUATA NAMUNGO KIBABE…ZAKA ZAKAZI AIBUKA NA HILI JIPYA…


KIKOSI cha Azam FC, kimeshuka mkoani Lindi, kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Namungo utakaochezwa keshokutwa Jumatano. Timu hizo mbili zitakutana kwenye Uwanja wa Ilulu, Lindi, huku Namungo walio kwenye kiwango bora msimu huu, wakiwa nyumbani kuwakaribisha Azam.

Timu hizo kwa sasa zote zina pointi 25, lakini Namungo ipo nafasi ya tatu ikiwa juu ya Azam iliyo nafasi ya nne, kutokana na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa. Mzunguko wa kwanza, Azam iliwafunga Namungo bao 1-0 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam, bao hilo pekee likifungwa na Mcongo, Idris Mbombo dakika ya 90.

Ofisa Habari wa Azam, Thabit Zakaria “Zaka Zakazi”, alisema wanataka kurudi Dar na pointi tatu muhimu.

“Tumeanza safari leo (jana) kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Namungo na tunaenda kupambana ugenini ili kuweza kurudi na alama tatu muhimu nyumbani.

“Wachezaji wote wapo vizuri kuelekea mchezo huo na morali ipo juu ili kuweza kurudi kwenye nafasi yetu Ligi Kuu Bara,” alisema Zaka.

SOMA NA HII  KUMBE SIMBA NI MBABE WA SINGIDA, TAKWIMU ZIPO HIVI