Home news BAADA YA KUSIKIA KESHO WAARABU WANASHUSHA ‘FULL MZIKI’…PABLO KAGUNA..KISHA AKAMTAJA MZAMIRU…

BAADA YA KUSIKIA KESHO WAARABU WANASHUSHA ‘FULL MZIKI’…PABLO KAGUNA..KISHA AKAMTAJA MZAMIRU…


KIKOSI cha Simba kinatarajiwa kuwa na mabadiliko makubwa katika mchezo wao wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane ya nchini Morocco kwa kumuingiza kiungo mtukutu, Mghana, Bernard Morrison.

Timu hizo zinatarajiwa kuvaana Jumapili hii saa 10:00 jioni katika mchezo wa Kundi D, ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo wa awali uliochezwa Morocco, Simba ilifungwa mabao 2-0, ambao Morrison alitokea benchi na kuleta mabadiliko makubwa katika kikosi hicho kwa kuwashambulia Berkane.

Mmoja wa mabosi wa Benchi la Ufundi la timu hiyo, amesema kuwa upo uwezekano mkubwa wa kikosi chao kuwa na mabadiliko katika safu ya kiungo katika mchezo huo dhidi ya Berkane.

Bosi huyo alisema kuwa mabadiliko hayo yatafanywa katika safu ya kiungo kwa kuwepo maingizo mapya ambayo ni Taddeo Lwanga, Mzamiru Yassin, Larry Bwalya na Morrison mwenyewe. Hawa watatu wa awali, waliukosa mchezo wa kwanza waliocheza Morocco.

Alisema kuwa uwepo wa viungo hao utawasaidia kimbinu kutokana na wapinzani wao Berkane kutowafahamu nyota hao ambao hivi sasa kambini wanaongezewa mbinu na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mhispania, Franco Pablo.

Aliongeza kuwa katika mchezo huo huenda baadhi ya viungo wakaanzia benchi ambao walikuwepo katika mchezo wa awali wa Morocco ambao ni Erasto Nyoni, Peter Banda, Kennedy Juma na Sadio Kanoute.

“Kama unakumbuka vizuri katika mchezo ambao tulicheza Morocco dhidi ya Berkane, robo ya wachezaji wetu muhimu wote wa kuanza katika kikosi cha kwanza walikuwa na majeraha.

“Hivyo alilazimika kupangua kikosi cha kwanza na kuwatumia mabeki wa kati kucheza nafasi ya kiungo ambao ni Kennedy na Nyoni ambao huenda katika mchezo huu wakaanzia benchi baada ya baadhi ya viungo kupona majerana na wengine kumaliza matatizo yao ya kifamilia.

“Kocha hivi sasa anawaandaa baadhi ya viungo ambao waliukosa mchezo wa ugenini kati ya hao yupo Lwanga, Bwalya, Mzamiru na Morrison ambaye alitokea benchi na kubadilisha mchezo kwa kuwashambulia wapinzani.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA MZIKI WA MUSONDA...STRAIKA SIMBA AWAPA YANGA UBINGWA MSIMU HUU...

“Hivyo huenda kikosi kitakachocheza mchezo huu ambao tutakuwa nyumbani, kikabadilika kwa kuwaanzisha viungo hao katika kuiimarisha safu ya kiungo ambayo Berkane wameonekana bora katika safu hiyo,” alisema bosi huyo.

Pablo alizungumzia hilo kwa kusema: “Mchezo wetu wa ugenini dhidi ya Berkane tuliwakosa wachezaji muhimu kutokana na matatizo mbalimbali ikiwemo majeraha na matatizo ya kifamilia.

“Hivyo ninafurahia kuona wachezaji wangu wote wakipona majeraha na kumaliza matatizo yao na niliwaandaa kwa kuwaongezea fitinesi katika mchezo wa ligi uliopita dhidi ya Dodoma Jiji ambao ni Bwalya, Mzamiru na Lwanga aliyetokea benchi dakika za mwisho kwa ajili ya kumuangalia,” alisema Pablo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here