Home news BAADA YA SIMBA KUTUA JANA KICHOVU…BIASHARA UTD WAITISHIA ‘NYAU’ ….WADAI WATAPIGA KWENYE...

BAADA YA SIMBA KUTUA JANA KICHOVU…BIASHARA UTD WAITISHIA ‘NYAU’ ….WADAI WATAPIGA KWENYE MSHONO…


KIKOSI cha Biashara United kitawasili Dar es Salaam kwa michezo miwili ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba na Ruvu Shooting.

Kocha mkuu wa timu hiyo, Mrundi Vivier Bahati alisema kuwa wamekuja kutafuta alama sita katika mechi hizo mbili ili kujikwamua kutoka nafasi za chini kwenye msimamo.

Hadi sasa Biashara ina pointi 15 ikishika nafasi ya 13 kwenye msimamo na inakutana na Simba yenye pointi 31 na ipo nafasi ya pili keshokutwa Alhamisi na baadaye itacheza na Ruvu Shooting inayoshika nafasi ya 12 kwa pointi 16.

“Tunahitaji alama tatu kwenye kila mchezo, tumekuja na wachezaji wote, na wanatambua umuhimu wa mechi hizo hivyo wapo tayari kwa kupambana,” alisema Vivier na kuongeza;

“Simba ni timu bora, tunaiheshimu lakini soka ni mchezo wa uwanjani, tunahitaji kushinda ndani ili kuongeza morali kwa wachezaji na kujikwamua huku chini tulipo.”

Biashara itaanza kucheza na Simba kwenye Uwanja wa Mkapa timu ambayo mzunguko wa kwanza wakiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Karume walitoka suluhu.

SOMA NA HII  RATIBA LIGI KUU YAANZA 'KUTIKISWA TIKISWA'...TPLB WATOA 'KAMKEKA' KAFUPI CHA MABADILIKO...SHOW ZIKO HIVI SASA..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here