Home Habar za Usajili Simba DAH…DILUNGA NDIO BASI TENA SIMBA…PABLO KAONA ISIWE TABU…KAMUONDOA JUMLA JUMLA…

DAH…DILUNGA NDIO BASI TENA SIMBA…PABLO KAONA ISIWE TABU…KAMUONDOA JUMLA JUMLA…


KUFUATIA majeraha ya muda mrefu ambayo ameyapata kiungo wa Simba, Hassan Dilunga, ambayo yanaweza kumuweka nje ya uwanja mpaka mwishoni mwa msimu huu, Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco, amefikia uamuzi wa kumuondoa nyota huyo kwenye mipango yake.

Akizungumza Kocha Pablo alisema: “Kuhusiana na Dilunga mwanzo hatukudhani angekuwa na jeraha kubwa ambalo lingemuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.

“Lakini kwa bahati mbaya tunaweza kumkosa labda mpaka mwishoni mwa msimu, hivyo tunalazimika kumuondoa kwenye mipango yetu kwa sasa mpaka pale taarifa za timu yetu ya madaktari itakapoonyesha kuwa yupo tayari kujiunga na timu.”

SOMA NA HII  KUMBE! WACHEZAJI WAMEMGOMEA MKUDE SIMBA