Home news DAKIKA CHACHE KABLA YANGA HAWAJASHUKA DIMBANI..HIZI HAPA SIKU 313 ZA NABI NA...

DAKIKA CHACHE KABLA YANGA HAWAJASHUKA DIMBANI..HIZI HAPA SIKU 313 ZA NABI NA PANDA SHUKA YAKE…


NAPOWAONA mashabiki wa Yanga wanatamba mtaani na mitandaoni ujue kuna jambo linalowatia kiburi hasa ikizingatiwa kwa misimu minne iliyopita wamepitia msoto wa maana katika Ligi Kuu Bara.

Anayewatia kiburi mashabiki hao ni Kocha Nasreddine Nabi ambaye kufikia leo anatimiza jumla ya siku 313 madarakani tangu aanze kuinoa timu hiyo.

Haya hapa mambo mbalimbali yaliyojitokeza ndani ya timu hiyo ikiwa chini ya kocha huyo Mbelgiji mwenye asili ya Tunisia aliyeanza kuinoa Yanga Aprili 25 mwaka jana alipoishudia Yanga ikipoteza mechi ya mwisho katika Ligi Kuu mbele ya Azam FC iliyowatungua bao 1-0.

MECHI 23 BILA KUPOTEZA

Mara ya mwisho kwa Yanga kupoteza mchezo kwenye Ligi Kuu Bara ilikuwa ni Aprili 25, 2021 dhidi ya Azam ilipofungwa bao 1-0, lililowekwa kimiani na Prince Dube kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Baada ya hapo wapinzani wamekiona cha moto huku mchezo wao wa mwisho Februari 27, 2022 walioichakaza Kagera Sugar 3-0 ulikuwa ni wa 23 kwenye Ligi Kuu, na kuifanya timu hiyo kutumia siku 313, bila kupoteza ikishinda mechi 18 na kutoka sare tao.

USHINDI MKUBWA

Ushindi mkubwa kwa Nabi tangu ajiunge na kikosi hicho cha ‘Wananchi’ katika Ligi Kuu Bara ni wa mabao 4-0, dhidi ya Dodoma Jiji Desemba 31, 2021 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

MABAO 38

Kwa msimu wa 2020/21, Yanga chini ya Nabi ilianza na ushindi wa mabao 2-0, dhidi JKT Tanzania Mei 19, 2021, (3-2) dhidi ya Ruvu Shooting na Mwadui Juni 17 na 20, 2021, (2-0) kutoka kwa Ihefu Julai 15, 2021, hivyo kufunga mabao 10 na kuruhusu manne.

Msimu huu wa 2021/22 imefunga mabao 28, katika michezo 16, ikiruhusu nyavu zake kutikiswa mara nne hivyo Nabi kuifanya timu yake kufunga jumla ya mabao 38 na kuruhusu nane.

MAKOCHA WANNE TU

Tangu ujio wa Nabi mabadiliko mengi yametokea kwenye benchi la ufundi ambapo katika timu 16, zinazoshiriki Ligi Kuu ni nne tu zilizosaliwa na makocha wao walewale ambao ni Boniface Mkwasa wa (Ruvu Shooting), Francis Baraza (Kagera Sugar), Malale Hamsini (Polisi Tanzania) na Mganda Mathias Lule wa Mbeya City.

SOMA NA HII  NABI AIHOFIA SIMBA FAINALI SHIRIKISHO

MAONI YA WADAU

Nyota wa zamani wa kikosi hicho, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ anasema moja ya mambo yanayoibeba Yanga msimu huu ni motisha iliyopo kwa wachezaji wao chini ya viongozi.

“Viongozi wamefanya kazi kubwa sana ukiangalia jinsi ambavyo timu inacheza inaonyesha ni kwa jinsi gani wamejipanga lakini huwezi kusifia tu bila kumpa heshima yake Nabi, kwani amechangia kuibadilisha na kucheza mchezo mzuri.”

Naye Sekilojo Chambua anasema: “Endapo Yanga itaendelea na kasi iliyopo kwa sasa, naamini watakuwa na msimu bora sana tofauti na misimu minne iliyopita kwani wameshaonyesha hilo kwa vitendo.”