Home Habari za Yanga HAWA HAPA MASTAA 5 WA YANGA WATAKAOKOSEKANA LEO..KAZE ASHINDWA KUJIZUIA…AFUNGUKA…

HAWA HAPA MASTAA 5 WA YANGA WATAKAOKOSEKANA LEO..KAZE ASHINDWA KUJIZUIA…AFUNGUKA…


WAKATI leo Machi 19,2022 vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga wakiwa na mchezo dhidi ya KMC kuna nyota wake wa kikosi cha kwanza ambao wanatarajiwa kuukosa mchezo huo.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa na utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zote kupiga hesabu ya kusepa na pointi tatu muhimu.

Miongoni mwa wachezaji ambao wanaweza kuukosa mchezo wa leo ni pamoja na Yacouba Songne, Jesus Moloko, Khalid Aucho, Said Ntibanzokiza na Chrispine Ngushi.

Nyota hawa hawapo fiti kutokana na kusumbuliwa na majeruhi ambayo waliyapata kwenye mechi za ushindani.

Cedrick Kaze, Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kuwa wanatambua mchezo wa leo utakuwa na ushindani mkubwa lakini wapo tayari kwa ajili ya kupata matokeo.

“Tunatambua kwamba mchezo utakuwa mgumu lakini tupo tayari kuona kwamba tunashinda, kikubwa ni mashabiki kuendelea kuwa pamoja nasi,”.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Majimaji, Songea ubao ulisoma KMC 0-2 Yanga.

SOMA NA HII  KISA MATOKEO YA TWAHA KIDUKU...MWAKINYO ASHINDWA KUJIZUIA...ATAJA WANAOMFELISHA...