Home news ISHU YA USAJILI WA ADEBAYOR SIMBA IKO HIVI…KUMBE WAMEPIGWA DANADANA..AHMED ALL AFUNGUKA…

ISHU YA USAJILI WA ADEBAYOR SIMBA IKO HIVI…KUMBE WAMEPIGWA DANADANA..AHMED ALL AFUNGUKA…


UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa dili lao la kumsajili winga hatari Mnigeria, Victorien Adebayor anayeichezea USGN ya Niger linaendelea vizuri kwa makubaliano ya mchezaji na wakala wake. Kinachofanyiwa kazi ni ruhusa ya wamiliki wa mchezaji huyo, Klabu ya HB Koge kutokea nchini Denmark.

Simba walivutiwa na Adebayor baada ya nyota huyo kuonyesha uwezo mzuri katika mchezo wao wa pili wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika, uliopigwa nchini Niger na kumalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1.

Adebayor ambaye mpaka sasa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika amefanikiwa kufunga mabao matatu katika michezo mitatu, kwenye kikosi cha USGN ya nchini Niger.

Akizungumzia kuhusu dili la staa huyo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema:

“Kwanza nadhani kila mmoja anakubali kwamba Adebayor ni miongoni mwa wachezaji bora, amethibitisha hilo katika michuano hii, ambapo wote tunajua kuwa alifunga mabao mawili dhidi ya Berkane kwao Morocco na hata sisi alitupa wakati mgumu.

“Ni kweli Simba ina nia ya dhati ya kumalizana na Adebayor ambapo baada ya mchezo wetu kule Niger, Mwenyekiti wetu wa Bodi, Salim Abdallah ‘Try Again’ alifanya mazungumzo na mchezaji mwenyewe na wakala wake ambao wote wamekubaliana na ofa yetu, lakini ishu tunayohangaikia kwa sasa ni ikiwa tunaweza kupata ruhusa ya klabu inayommiliki kule Denmark kwa kuwa sasa yupo USGN kwa mkopo.”

SOMA NA HII  NYIE CHONGEENI LAKINI YANGA WAMEPANIA...WATU 41 KUWAFUATA WAARABU KIBABE KESHO...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here