Home Habari za michezo JERRY MURO:- “MANARA SIO MWANAYANGA….HASIRA ZIKIMWISHA ATARUDI ALIKOTOKA…”

JERRY MURO:- “MANARA SIO MWANAYANGA….HASIRA ZIKIMWISHA ATARUDI ALIKOTOKA…”


Mkuu wa Wilaya ya Ikungi ambaye aliwahi kuwa msemaji wa klabu ya Yanga, Mhe. Jerry Muro amesema anaamini Haji Manara akipewa muda atafanikiwa japokuwa anaamini si mwanachama halisi wa klabu hiyo.

“Ameanza tumpe muda naamini atafanya vizuri kama amekuja kwa nia ya dhati, na kama amekuja kwa hasira itatusaidia kutusogeza na pale hasira itakapoisha huenda akarudi alikotoka”, amesema Mhe. Muro.

“Kila mtu anajua Haji ni do or die mwanachama wa Simba, Haji siyo mwanachama wa Yanga amekuja kutafuta riziki au mkate wake”, ameongeza.

SOMA NA HII  SIRI YA AZAM FC KUSAJILI WASHAMBULIAJI YAFICHUKA...USAJILI WA FEI TOTO WATAJWA...