Home news KISA SIMBA…VIGOGO WAVAMIA KAMBI YA YANGA KIGAMBONI..MAKAMBO ATOBOA SIRI A-Z…..DK MSOLA ‘ALIA’..

KISA SIMBA…VIGOGO WAVAMIA KAMBI YA YANGA KIGAMBONI..MAKAMBO ATOBOA SIRI A-Z…..DK MSOLA ‘ALIA’..


VIGOGO wa Yanga wakiongozwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Dk. Mshindo Msolla juzi walitimba kambi ya kikosi hicho na kufanya kikao kizito na wachezaji, kubwa ni kupeana michongo mizima ya kuhakikisha msimu huu wanabeba ndoo ya Bara.

Yanga kwa misimu minne mfululizo imekuwa ikitoka kapa kwenye Ligi Kuu Bara, lakini safari hii mabosi wa klabu hiyo wamegoma kuwaachia watani wao Simba kubeba tena ndoo ya msimu huu na ndipo juzi wakaamua kutinga kambini na kuteta na wachezaji wao wakipeanda mikakati ya kulirejesha taji Jangwani.

Ipo hivi. Dk Msolla akiambatana na wengine wakiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano, Rogers Gumbo na Mwenyekiti wa kamati ya ufundi, Dominic Albinus kufanya kikao kizito na wachezaji wao.

Mabosi hao wa Yanga walitinga ilipo kambi ya Yanga, Avic Town Kigamboni na kufanya kikao kizito na wachezaji, benchi la ufundi kilichozungumzwa mambo muhimu matano ndani yake.

Inaelezwa kuwa, Dk. Msolla ndiye alikuwa akizungumza na jambo la kwanza aliwapongeza wachezaji na benchi la ufundi kwa kazi kubwa waliyoifanya mpaka mzunguko wa kwanza unamalizika wakiwa vinara wa ligi.

Baada ya pongezi hizo Msolla aliwakumbusha wachezaji na benchi la ufundi kuwa msimu uliopita mpaka duru la kwanza linaisha walikuwa vinara wa ligi lakini duru la pili walishindwa kumaliza vyema na kushindwa kutwaa ubingwa.

Jambo la pili, mwenyekiti huyo aliwaambia duru la kwanza wamepoteza pointi sita ili kufikisha zile 45 kama wangeshinda michezo yote, hivyo duru hili la lala salama wachezaji na benchi la ufundi wanatakiwa kupambana vya kutosha na kama watapoteza pointi zisiwe zaidi ya sita.

Pia aliwaambia kwenye duru la pili kila mechi itakuwa ngumu zaidi na ushindani wa kutosha kutokana na wapinzani wao hawatakubali kufungwa mara mbili, pia wanahitaji pesa za udhamini wa ligi na kila moja inapambana kumaliza vizuri.

Baada ya hapo kila mchezaji aliambiwa anapaswa kupambana kadri ambavyo anaweza kulingana na majukumu ya nafasi yake na kuhisi Yanga msimu huu inahitaji mafanikio.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA OFA YA GOR MAHIA KWA ONYANGO....SIMBA 'WAIJIBU KITAJIRI'...WATAKA DAU NONO...

Mwisho Dk. Msolla aliwaeleza uongozi upo nao bega kwa bega katika kila jambo kuhakikisha msimu huu wanatwaa ubingwa wa ligi waliyoukosa misimu minne pamoja na kutwaa ubingwa wa kombe la Shirikisho (ASFC).

Msimu uliopita Yanga ilimaliza duru la kwanza ikikusanya pointi 37, ikiitangulia Simba kwa tofauti na pointi mbili, lakini mwishoni mwa msimu ikajikuta ikimaliza ya pili na pointi 74 na Simba ikibeba ubingwa mwa msimu wa nne mfululilo ikikusanya alama 83. Kwa msimu huu Yanga imemalizia duru la kwanza na pointi 39 baada ya mechi 15, huku Simba ikiifuata na pointi 31.

WASIKIE SASA

Mshambuliaji Heritier Makambo alisema mara nyingi wanapotembelewa na viongozi, huwapa morali na hali ya kushindana zaidi katika kila mechi iliyokuwa mbele yao.

“Jambo kubwa kwetu hilo wamelifanya kwani tunaamini tupo pamoja na viongozi na wanatambua kile ambacho tunakifanya uwanjani,” alisema, Makambo huku Meneja Hafidh Saleh alisema jambo hilo la kawaida kwa viongozi kuwapa maneno yenye ujumbe mkubwa ndani yake ni kama Baba kwenye familia anapomueleza mwanae akasome vizuri.