Home news KUELEKEA MECHI YA LEO DHIDI YA DODOMA JIJI….SIMBA WATOA TAARIFA KUHUSU HALI...

KUELEKEA MECHI YA LEO DHIDI YA DODOMA JIJI….SIMBA WATOA TAARIFA KUHUSU HALI YA KAPOMBE…


Klabu ya Simba imewatoa hufu Mashabiki na Wanachama wake kuhusu hali ya Beki wa kulia wa kikosi cha klabu hiyo Shomari Salum Kapombe, baada ya kupata majeraha akiwa kwenye mchezo wa Juzi Ijumaa (Machi 04).

Simba SC ilikua mwenyeji wa Biashara United Mara Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam, na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0  yaliyofungwa na Viungo Mzamiru Yassin, Clatous Chama na Pappe Ousmane Sakho.

Kapombe hakumaliza mchezo huo, baada ya kugongwa usoni na mchezaji wa Biashara United Mara katika kipindi cha kwanza, na nafasi yake ilichukuliwa na Israel Mwenda.

Simba SC imethibitisha kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuhusu hali ya Beki huyo, ambaye alilazimika kuondolewa uwanjani akiwa kwenye machela.

Taarifa iliyobandikwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii ya Simba SC inasomeka: Beki bora wa kulia nchini yuko 👍🏽 Jumatatu shoo kubwa itaendelea kwa Mkapa. #NguvuMoja.

Kwa maelezo hayo, Shomari Salum Kapombe yupo FIT na huenda akawa sehemu ya kikosi cha Mabingwa hao wa Tanzania Bara katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji FC utakaopigwa leo Jumatatu (Machi 07), Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.

Ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Biashara United Mara, umeiwezesha Simba SC kufikisha alama 34 zinazoiweka katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, huku Young Africans wakiendelea kuwa kileleni kwa kumiliki alama 45.

SOMA NA HII  UZI MPYA WA TAIFA STARS HUU HAPA....SERIKALI WAPIGA MKWARA WA 'KUFA MTU'....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here