Home Habari za michezo MASOUD :- WACHEZAJI ACHENI KUZITAMANI SIMBA NA YANGA…MIRAJI ATHUMAN KAWA ‘BONGE NYANYA’..

MASOUD :- WACHEZAJI ACHENI KUZITAMANI SIMBA NA YANGA…MIRAJI ATHUMAN KAWA ‘BONGE NYANYA’..


Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji, Masoud Djuma amewataka wachezaji wenye umri mdogo ambao wana malengo ya kucheza Simba na Yanga, watengeneze kwanza viwango kabla ya kukimbilia pesa.

Djuma ambaye amewahi kuwa kocha msaidizi wa Simba, alisema wachezaji wengi wa Tanzania wana vipaji lakini wamekuwa wakikimbilia kucheza timu hizo kongwe kwa sababu ya pesa, kabla hawajaboresha viowango vyao hivyo kuviua kabisa, kutokana na wakati mwingine kutopata nafasi ya kucheza.

“Wengi wanaharibu soka lao hivyo. Mchezaji kama Miraji Athuman nimwemwangalia kama mfano. Alikuwa mfungaji mzuri lakini sasa amekuwa bonge, hawezi kucheza tena,” alisema na kuongeza;

“Kule kunahitaji aliyekamilika, wasiwe na tamaa ya fedha wasubiri wakomae ndio waende, muda utafika. Timu kubwa zina presha, unaenda pale haujakomaa kisoka ni kama vile unaenda kuhemea chakula, ndizi mbivu unataka kuila muda huo huo subiri iive.”

“Simba, Yanga na Azam kuna wachezaji wengi wengine wanacheza timu za taifa. Utawezaje kumtoa mchezaji pale. Kule unaweza ukapata pesa lakini kiwango kikashuka. Hivyo, nawashauri watengeneze kwanza viwango ndipo watapata nafasi ya kucheza na pesa,” alisema

Kuhusu kiungo wake, Cleophace Mkandala ambaye amekuwa akisakwa na timu mbalimbali, amemshauri kuwa na utulivu katika kipindi hiki.

“Ni mchezaji kiungo, hata mimi nilikuwa nacheza katikati, ana kipaji kikubwa halafu hataki kukitumia, namkosoa kwa hilo. Ana mambo mengi anaweza akaleta katika timu. Anajua mpira na ana miaka mingi ya kucheza, asipoitumia vizuri atapata shida,” alisema.

Kuhusu timu yake alisema; “Nimekuta haina matokeo mazuri. Kuna mengi ya kufanya. Nataka kuirudisha ipate matokeo mazuri,” alisema.

SOMA NA HII  YANGA INAGAWA DOZI NYUMBANI NA UGENINI...GARI LIMEWAKA JANGWANI...MNYAMA HAFUI DAFU