Home news WAKATI SIMBA NAO WAKIZIDI KUTAKATA LIGI KUU…AHMED ALLY ‘KAWACHUNGULIA YANGA’..KISHA AKASEMA HAYA…

WAKATI SIMBA NAO WAKIZIDI KUTAKATA LIGI KUU…AHMED ALLY ‘KAWACHUNGULIA YANGA’..KISHA AKASEMA HAYA…


VIONGOZI wa Simba wanaamini kuwa ubingwa wa ligi kuu bado ni mali yao na hakuna namna yoyote ya timu nyingine kuchukua ubingwa huo.

Mbali na viongozi, hata Kocha wa Simba, Pablo Franco Martin, amesema kuwa asilimia za timu yake kutetea ubingwa bado ni nyingi kwa kuwa safari ya kuwania ubingwa bado ipo wazi.

Pablo alisema, kila hatua wanayoipiga inakuwa na malengo makubwa na hata kila kwenye mechi ya ligi kuu, wana malengo ya kutwaa ubingwa huo hata kama wapo nyuma kwa alama nyingi. 

“Ubingwa bado upo wazi na kila timu ina nafasi na hata wao wanaweza kutwaa ubingwa na ndiyo mpango walionao msimu huu.”

Kwa upande wa Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Ahmed Ally, alisema uongozi wa klabu hiyo umepanga mpango Madhubuti wa kuhakikisha ubingwa unabaki Simba.

“Kila kitu kipo kwenye ‘set’ kwa maana kuna mpango maalumu umepangwa na uongozi wa klabu yetu ili kuhakikisha kuwa ubingwa kwa mara ya tano unakuja Simba.

“Hao waliotangulia hawana lolote na hawawezi kututisha kwa sababu ndiyo staili yao, wanatangulia na lori na sisi tunakuja kuwapita na Range Rover,” alisema.

SOMA NA HII  BAADA YA KUPOKEA KICHAPO LEO....NABI AVUNJA UKIMYA YANGA...AFUNGUKA WALIMUANGUSHA...