Home news WAKATI TETESI ZA KUUZA MECHI KWA YANGA ZIKIZIDI KUVUMA…GEITA GOLD WAVUNJA UKIMYA…WAIBUKA...

WAKATI TETESI ZA KUUZA MECHI KWA YANGA ZIKIZIDI KUVUMA…GEITA GOLD WAVUNJA UKIMYA…WAIBUKA NA HILI…


Uongozi wa klabu ya Geita Gold FC umetangaza msimamo wa kutokua tayari kuuza mchezo wake dhidi ya Young Africans utakaopigwa kesho Jumapili (Machi 06), katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Uongozi wa klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya kwanza msimu huu 2021/22, umetoa taarifa za kutokua tayari kufanya hivyo, kufutia tetesi zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii, zikieleza Geita Gold FC imeuza mchezo huo.

Taarifa hizo zimesisitiza kuwa Uongozi wa klabu hiyo ya mkoani Geita umeamua kuuhamisha mchezo wao dhidi ya Young Africans kutoka Uwanja wa Nyankumbu na kuupeleka CCM Kirumba Jijini Mwanza ili iwe rahisi kwa wapinzani wao kupata matokeo.

Mtendaji Mkuu wa Geita Gold Simon Shija, amesema katu klabu hiyo haiwezi kufanya mchezo huo mchafu na wanashangazwa kuona taarifa hizo kwenye mitandao ya kijamii, huku akisisitiza zina lengo la kulichafua soka la Tanzania.

Amesema lengo la kupeleka mchezo huo katika Dimba la CCM kirumba ni kutokana na Masuala ya kiusalama kuhofia mashabiki kujaa endapo wangechezea katika Dimba lao la Nyankumbu Mkoani Geita.

“Hapa kuna taarifa ambazo sio rafiki kwa soka letu la Tanzania, kwa hakika zimetushangaza sana kwa sababu sio desturi ya nchi hii kuzungumzwa katika mazingira ya kuuza mchezo wa soka ama mchezo wowote ule,”

“Dhumuni letu la kuuhamisha mchezo huu, tumezingatia sana suala la kiusalama kwa mashabiki ambao tulihofia kama tungecheza nyumbani katika Uwanja wa Nyankumbu, huenda hali ingekua mbaya, hivyo tumeamua kuupeleka Mwanza ili kuondokana na kadhia hiyo ambayo tumeizingatia kwa kuepuka changamoto ambazo zingejitokeza.”

Aidha Shija amewataka mashabiki kuendelea kujitokeza kwa wingi kununua tiketi katika maeneo mbalimbali huku akiwataka kuja katika dimba la CCM kirumba kushabikia timu yao.

“Mchezo huu katika kanda ya Ziwa ni wetu sote, Mashabiki wanapaswa kufika kwa wingi Uwanjani kwa ajili ya kushuhudia soka la ushindani ambapo tunaamini timu iliyojiandaa vizuri itashinda na sio mambo mengine yanayoendelea kusambazwa kwa mipango ya kutuchafulia soka letu.” amesema Shija

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUKABIDHIWA RUNGU LA USAJILI..NABI AVUNJA UKIMYA..ATUPA KOMBORA KWA UONGOZI...

Katika mchezo wa Duru la Kwanza la Ligi Kuu msimu huu uliozikutanisha timu hizo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, Young Africans ilichomoza na ushindi wa bao 1-0, lililofungwa na Kiungo Mshambuliaji Jesus Moloko.

Young Africans inaendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 42, huku Geita Gold FC yenye matokeo ya mazuri kwa siku za karibuni ikiwa na alama 21 zinazoiweka katika nafasi ya 07 kwenye msimamo.