Home KMC FC WAKATI YANGA WAKICHEZA NA WASOMALI …KMC WAONA ISIWE TABU…HITIMANA ‘AJICHONGEA RUNGU LA...

WAKATI YANGA WAKICHEZA NA WASOMALI …KMC WAONA ISIWE TABU…HITIMANA ‘AJICHONGEA RUNGU LA KUUA’


Mara baada ya kumalizika kwa mapumziko ya siku moja kikosi cha KMC FC  kimeanza tena maandalizi ya kujiandaa na mchezo mwingine wa 18 wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania bara dhidi ya Yanga utakaochezwa siku ya Jumamosi ya Machi 19 katika uwanja wa Benjamini Mkapa hapa Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo muhimu Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni chini ya kocha Mkuu Thierry Hitimana itakuwa ugenini ikiwa ni baada ya kumalizika kwa mchezo wa mzunguko wa 17 dhidi ya Coast uliopigwa siku ya Jumatatu ya Machi saba katika uwanja wa Azam Complex na kupoteza kwa mabao matatu kwa mawili.

KMC FC imesaliwa na siku nane za kujiandaa na mchezo huo na kwamba katika kipindi hichi Kocha Mkuu Hitimana ameandaa program ya mazoezi mbalimbali sambamba na kucheza mechi za kirafiki ambazo zitakuwa muhimu kwa ajili ya kuwaweka wachezaji katika hali nzuri.

Katika maandalizi hayo, KMC FC inafahamu kuwa inakwenda kucheza na Timu ambayo inaongoza ligi kwa sasa na kwamba kila mmoja anatambua,ugumu na ushindani utakaokuwepo katika mchezo huo lakini hiyo haitazuia Kino Boys kupata matokeo mazuri kutokana na ubora wa wachezaji wa Timu hiyo.

 “Tunakwenda kwenye mchezo muhimu ambao kimsingi tunafahamu utakuwa na ushindani mkubwa, lakini pamoja na ushindani huo haimanishi kuwa KMC tutashindwa kupata matokeo, kimsingi kila mmoja anahitaji ushindi na kwamba kila siku tumekuwa na maandalizi bora kwa kila mchezo ambao unakuwa mbele yetu.

Ukiangalia ratiba ya mchezo wetu ni Machi 19, leo ni tarehe 09, kwa hiyo tunakaribu siku tisa za kufanya maandalizi yetu,  kikubwa ni kujipanga vizuri, kuzitumia vizuri sikuhizi za mazoezi, tunaamini kuwa tutakuwa bora kwenye mchezo huo na hivyo kufanya vizuri kutokana na ubora wa benchi la ufundi pamoja na wachezaji tuliliokuwa nao.

KMC FC hivi sasa ipo katika nafasi ya sita ikiwa imecheza michezo 17,nakushinda michezo mitano, sare michezo saba huku ikipoteza michezo mitano na hivyo kukusanya jumla ya alama 22 muhimu na kwamba bado inahitaji kupanda zaidi kwenye nafasi tatu za juu.

SOMA NA HII  SIKU CHACHE BAADA YA KUFUKUZWA ...ADEL ZRANE AIBUKA NA KUFICHUA YA SIMBA...AGUSIA USAJILI ...

Imetolewa Machi 09

Na Christina Mwagala

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here