Home CAF AMSHA AMSHA ZA MASHABIKI SIMBA ZAMTISHA STAA WA ORLANDO…ADAI WANA HOFU ‘KIMTINDO’…

AMSHA AMSHA ZA MASHABIKI SIMBA ZAMTISHA STAA WA ORLANDO…ADAI WANA HOFU ‘KIMTINDO’…


Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Malawi na klabu ya Orlando Pirates ya nchini Afrika Kusini, Hellings Frank “Gabadinho” Mhango anaamini Mashabiki wa Simba SC ndio sababu kubwa ya klabu hiyo kupata ushindi kila inapocheza katika Uwanja wa Nyumbani (Benjamin Mkapa Stadium.)

Simba SC imekua na sifa ya kipekee miongoni mwa klabu za Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, ya kushinda michezo yake ya Kimataifa inapocheza nyumbani, hali ambayo imeleta hofu kwa wapinzani wanaocheza nao Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Gabadinho ambaye ni miongoni mwa wachezaji waliowasili jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo tayari kwa mchezo wa Mkondo wa Kwanza Hatua ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba SC, amesema Mashabiki wa klabu hiyo wamekua silaha kubwa ya ushindi ambayo siku zote imekua kikwazo kwa timu inapocheza katika Uwanja wa ugenini.

“Sio kwamba ninafahamu sana kuhusu soka la Tanzania, lakini tayari tumeona vitu vingi kuhusu Simba na tunaifuatilia kwa kuwa ndio timu ambayo tutapambana nayo basi ilikuwa lazima kuangalia kuhusu nguvu yao ipo wapi.”

“Kuhusu hofu juu yao tutakapocheza nao kesho Jumapili wakiwa nyumbani nadhani si sana japo mara nyingi katika michuano hii timu ambazo zimekuwa zinafanya vizuri ni zile zinazokuwa nyumbani, lakini tutapambana kuhakikisha tunafanya vizuri katika mchezo huo,” amesema Gabadinho.

Katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu huu 2021/22, Simba SC imecheza michezo mine dhidi ya Red Arrows ya Zambia, ASEC Mimosas ya Ivory Coast, RS Berkane ya Morocco na USGN ya Niger na kushinda yote.

Katika mchezo Robo Fainali kesho Jumapili (April 17), Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), limeiruhusu Simba SC kuingiza mashabiki 60,000 ambao ndiyo idadi kamili wanaoingia Uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  KUHUSU SIMBA KUFIKA FAINAL YA CAF...ZIMBWE Jr AWAPIGA 'BREKI' WANAOWAZA HIVYO...ATAJA HATUA HIZI..