Home Habari za michezo BAADA YA KUICHAPA USGN KIPOGO CHA ‘MWANA UKOME’…..AHMED ALLY AMRUSHIA MANARA KIJEMBE…

BAADA YA KUICHAPA USGN KIPOGO CHA ‘MWANA UKOME’…..AHMED ALLY AMRUSHIA MANARA KIJEMBE…


Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amewapiga kijembe watani zao wa jadi Young Africans, baada ya kikosi chao kutinga Hatua ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Simba SC iliibanjua USGN mabao 4-0 jana Jumapili (April 03), Uwanja wa Benjamin Mkapa na kufikisha alama 10 zinazoivusha kwenda Robo Fainali.

Ahmed ameandika ujumbe huo huku akificha jina la Young Africans, lakini ametumia jina la jirani ambalo ni dhahir linamaanisha Watani zao wa Jadi.

Ahmed ameandika kupitia ukurasa wake wa Instragram: Huu ndo mzuka wa kimataifa!!!πŸ”₯

Usiku wa mnyamaa ulipendeza haswa

Huwezi amini kama hapo ni Benjamin Mkapa huo Moshi ndo unazalisha pumzi ya moto, wapinzani wakachanganyikiwa mpaka wakajifunga

Aisee majirani Kumbe mnajua kunyamaza EeehπŸ˜„πŸ˜„

Kumbe mnajua kuacha kutukana kwenye page za watu πŸ˜„πŸ˜„

Mpoo kimyaaaaa au mmefariki wote semeni kitu basi hatujawaozea hivyo πŸ˜€πŸ˜€

Inafahamika kuwa , Manara na Ahmed Ally ni watani, ambapo mara kadhaa wamekuwa wakicharurana mitandaoni kwa mafumbo ya hapa na pale.

Alama 10 zimeifanya Simba SC kushika nafasi ya pili katika Msimamo wa β€˜Kundi D’ sawa na RS Berkane inayoongoza kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

RS Berkane wamefikisha alama 10 baada ya kuifunga ASEC Mimosas ya Ivory Coast 1-0, mjini Berkane-Morocco jana Jumapili (April 03).

SOMA NA HII  BAADA YA KUANZA KUTUPIA SIMBA...OKRAH ATOA UJUMBE HUU KWA MASHABIKI NA KWA KOCHA MPYA....